Kuhusu madaraka ya DC

jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,401
4,965
Nadhani kuna haja ya kufafanuliwa kwa kina madaraka ya DC au hata rais kuweka watu ndani yakoje kisheria. Nadhani watu wengi tumelewa mahaba ya "hapa kazi tu" tunashindwa kuona matishio ya kutumia madaraka haya vibaya. Nilivyokuwa najua ni kuwa maamuzi haya hufanyika pale ambapo kuna tishio la amani tu na sio kutumika kana kwamba DC au rais ni mungu mtu!
Mfano, waumini wa makanisa ni wananchi wa Tanzania wenye haki zote kikatiba za kwenda kushitaki polisi/mahakamani kwa jambo lolote lile kwa mujibu wa sheria. Inakuwaje haki hizi ziminywe kwa tishio la kuwekwa ndani kwa kuwa tu DC hapendi? Kuna mambo mangapi ambayo yanaweza kuwa sahihi kikatiba lakini DC asiyapende? Je ni sahihi kuwa ana madaraka ya kuweka ndani watu kwa sababu wanapingana na utashi wake? As simple as that?
 
Kasome Report ya Tume ya Justice Nyalali kuhusu sheria 40 kandamizi ambazo zikistahili kufutwa ama kurekebishwa. Sijui ni ngapi zimerekebishwa hadi sasa ila nakumbuka hiyo ya kutia watu ndani kwa MaDC na Ma RC ilikuwa mojawapo. Sheria ya nguvu kazi pia bado ni hai na unaweza kamatwa na Polisi na kutiwa ndani kwa kosa la kuzurura !!!
 
Back
Top Bottom