Kuhusu kombe la dunia

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
Producer wa Wimbo wa Kombe la Dunia (Official theme song) anaitwa RED ONE ni mzaliwa wa Morocco.

Wimbo huo unaitwa Hayya Hayya (Better Together) umeimbwa na Trinidad Cardona (America) akimshirikisha Davido (Nigeria) na Aisha (Qatar) ulitoka 1 April 2022.

Pia aliyechonga Kombe la Dunia la Mwaka huu, achana na lile OG, ni hili la replica material anaitwa Ahmed Ait Sidi Abdelakder mzaliwa wa Morocco.

Kila Baada ya Miaka Minne kombe la Dunia OG, lazima lirudi lilikochongwa (Italy) katika kampuni ya Bertoni.

Kampuni hiyo ndio Hutengeneza makombe mengine Ahmed alipohojiwa alisema
"Replica si dhahabu bali shaba, Tunafanya kwa ajili ya macho, Tumetengeneza vikombe vingi hapa, kwa ajili ya Afrika,Ulaya,Amerika,Lakini hili la mwaka huu lina athari ya kipekee, tofauti na nyingine zote".

Kumbuka Kampuni hii ya Bertoni ndio ilichonga UEFA Cup trophy, UEFA Super Cup, Olympic Order, Arabian Gulf Cup moja ya kazi kubwa kabisa na zinazofahamika (Notable work).

Pia nchi ya Morocco Itaisaidia Qatar katika Usalama wakati wa Kombe la Dunia, Qatar imetoa taarifa ya pamoja ikiahidi kuongeza usalama kupitia kikundi cha cybersecurity agents kutoka Morocco, Ombi la Qatar ni kusaidiwa kuimarisha usalama katika Uwanja wa Lusail Iconic Ambako mechi ya fainali ya Kombe la Dunia itachezwa, Pia Afisa Kurugenzi Kuu Ya Ufuatiliaji wa Usalama Wa Kitaifa Morocco (DGSN-DGST) anayeitwa Abdellatif Hammouchi yuko Qatar kwa Ajili mazungumzo ya Kuongeza Ulinzi wakati wa Kombe la Dunia (Morocco’s assistance)

Polycarp Mdemu

FB_IMG_1665225999953.jpg
 
Back
Top Bottom