Kuhusu kanzidata (database) ya Sekretarieti ya Ajira

Kuhusu kanzidata (database) ya Sekretarieti ya Ajira

Dah yawezekana database huwa inaexpire, me Ina zaidi ya mwaka kimya, na wenzangu wameitwa last time mwezi wa 7 mwaka jana
Mkuu wakat wako bado haujafika usikate tamaa siku yako itafika soon
 
Dah yawezekana database huwa inaexpire, me Ina zaidi ya mwaka kimya, na wenzangu wameitwa last time mwezi wa 7 mwaka jana
Data base ina mida maalum wa kutunza nadhan Ni mwaka mmoja,na kuwekwa kwenye kanzi data so guarantee kuwa ndo utapata kazi ndo maana hawawez kuweka majina hadharani,ukiona kazi uloyofanyia interview wameshachaguliwa watu Basi ridhika Mambo ya kanzidata Ni majaaliwa tu,na Ni Bora usijipe stress kuiwaza maana hutaweza kufanya interview nyingine vZr!
 
Interview ulifanya lini na jina limetoka lini kwenye tangazo la ajira?

Kaka kwanza pole kwa unayopitia ila naomba nikutie moyo endelea kupambana usikate tamaa na naongea aya coz nina ushuuda mm mwenyewe nilifanya written pia nikafaulu nikaitwa oral lakini nafasi husika nilizofanyia pepa wala sijapata na nilijua wakat natoka kwenye interview ya oral lazima nipate nafasi yangu ila mungu si athumani sikukata tamaa kabisa juzi tu nimeona jina langu kwenye portal ya utumishi so pambana usiache kumuomba mungu kila la kheri ndugu
Kaka hivi ukiwa unasubiri kule kwenye status inasomekaje?
 
Kwanza napenda kuipongeza sekretarieti ya ajira kwa kuwasaidia vijana ( watoto wa wakulima ) kupata ajira serikalini sababu bila ya nyinyi hali ingekua ngumu sana kwa sisi walalahoi kupata ajira serikalini.Nasema hivyo kwasababu taasisi nyingi za serikalini zimejaa undugu kiasi kwamba huwezi kupata kazi bila ya kuwa na mtu unaemfahamu katika taasisi unayotaka kuomba kazi.

Sekretarieti ya ajira imekua na utaratibu wa kuendesha usaili kwa kada mbalimbali na wanaofaulu hupangiwa vituo vya kazi.Kwakua nafasi zinakua finyu wale ambao wamefaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi majina yao huifadhiwa kwenye kanzidata (database) kama majina ya reserves(akiba).

Kitu ambacho nadhani wanachotakiwa kufanya ni kuweka hadharani majina ya waliopangiwa vituo vya kazi na vilevile waweke wazi majina ya wale ambao wameingia kwenye database ili nao wawe na matumaini flani hata kama ikitokea sio wote watakaopata nafasi lakini angalau wajue kwamba ni wangapi wameingia kwenye database.

Kwakumalizia napenda kuwapongeza kwa kuwasaidia watoto wa wakulima ambao hawana wa kuwashika mkono katika mchakato mzima wa kupata ajira serikalini.

Asante.
Nadhani haitaleta afya kwani kukaa kwenye database sio tiketi ya moja kwa moja ya kupata ajira.Hii ni kwa sababu database inaweza kuisha muda na nafasi haipo,sasa utampa mtu matumaini ya bure akabetweka asiombe ajira zingine kisa anasubiri database
 
Nadhani haitaleta afya kwani kukaa kwenye database sio tiketi ya moja kwa moja ya kupata ajira.Hii ni kwa sababu database inaweza kuisha muda na nafasi haipo,sasa utampa mtu matumaini ya bure akabetweka asiombe ajira zingine kisa anasubiri database
Mimi naona ni vyema kama hujapa ajira na tayari upo kwenye kanzidata usiache kuendelea kuomba ikiwa tu system haikatai
 
Kuna moja ya Tantrade nilikisha siku 4 mfululizo nakumbuka nilikuwa the best..

Baada ya oral, sijui ilikuwaje ase..
Kwanza wanasema Tantrade walipeleka watu wao badala ya watu waliokuwapo kwenye mchakato
Ulijuaje km ulikuwa best haliyakuwa matokeo ya oral hayatangazwi?Vipi uliwahi kuwauliza kupitia simu zao?
 
jaman tunapenda kulalamika sana...wakitoa majina yaliyopo kwenye database halafu usipoitwa utaanza kulalamika....xo hatuhitaji kuyajua na lengo letu ni kupata ajira husika na sio kuingia kwenye database...kuingia kwenye database ni huruma yao tu..na inapotokea kuna shirika linataka mtu na halitaki gharama za interview ndo linachukua mtu kwenye database kama yupo..basi wafanye ukishindwa umeshindwa tu....maana tunalalamika....mbona hatulaumu na private waweke database
Naunga mkono hoja. Cha msingi mchakato uwe mfupi tu maswala kujua kama upo database italeta shida kubwa sana.
 
Back
Top Bottom