My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,293
Wakuu salamu,
Kuna tetesi zimeenea ya kwamba PPF wameanza kutoa fao la kujitoa, je? Kuna ukweli wowote katika hilo wakuu? Maana nilipoona nimedhulumiwa nikaamua kuondoka na kwenda zangu Kenya kufanya biashara.
Kama kuna ukweli wakuu naomba tujuzane ili nije nichukue ka cent kangu na miye jamani. Na endapo si kweli basi PPF imejipalia kaa la moto, itakuja kufa kifo cha mende, na wala isibweteke kwa wafanyakazi wachache hasa wa sekta za umma ilionao, sasa hivi wafanyakazi wa sekta binafsi hawataki kabisa kusikia kuhusu PPF, unapowatajia PPF ni kama unawatajia chumba cha maiti.
Ni ajabu sana kumdhulumu mtu maskini, ndo maana hatuendelei kwa laana. Hivi mtu kila mwezi anakatwa kodi, mafao yake ya mwisho ndo yanayomweka mjini, hayo mafao ni jasho lake na mwajiri wake.
Nyie kwa sababu mna bunduki na mabomu bila huruma mnatangaza kufungia pesa za watu, mna tofauti gani na majambazi nyie? Maana mtu akitumia nguvu kuwadai hawezi kusalimika. Mimi binafsi nina mil 38.9 nazowadai PPF, pesa hizi ni nyingi mno.
Katika mataifa yaliyoendelea, mfanyakazi hapewi mafao yake ila akikosa kazi hupewa ama kutafutiwa kazi na shirika husika, sasa nyie mnapora mafao ya watu bila compensation yoyote ni nani atakubali huo ujambazi wenu?
Hebu tazama hizo pesa uone kama ni rahisi kihivyo mtu kukupora, jiangalie Sana nyie watu, kutueleza eti hadi tufikishe miaka 55, unawezaje kupanga pesa ya mtu itumikeje? Narudia tena, jasho la mtu huwa haliliwi, na wala haliendi bure, so watch out you guys.