Kuhusu ACT - Tanzania

Mkuu sikuwahi fahamu kuwa wewe ni mtupu kiasi hiki....ukisoma vizuri ufafanuzi wako utajiona ni kwa kiasi gani wewe ni mfuasi wa unayoyapinga na mbaya zaidi mwenye wivu wa kike...
1. I thought u cld tell JF members that ur among the founder of this new part but ur just narating and advertising weakness of other parts?
2؛‎ urr just posion mongers and rumor mongers....any serious institution will not accomodate u as always u grade urself a perfect creature in politics of Tanzania..
3. U will remain a traitor even in ur family for the if u will not change ur vision
Tunawatakia mafanikio mema wasaliti katika chama chenu kipya...najiuliza mlivyo weupe nani atakuwa chair....
Nimeyapima maneno yako nakuona kama defensive, Kuna kitu umeguswa na unashindwa kukisema lakini ukweli demokrasia inaweza kukuweka juu au ikakuporomoa, inategemeana umeitendea nini(umeipoka au umeiruhusu ifanye kazi)
Jipime.
 
Naulizwa sana kwenye inbox na simu kuhusu ukweli wa hiki chama mpya cha ACT-Tanzania,

Majibu yangu ni Mafupi tu kama yafuatayo:-

i) Kwanza kabisa siwaungi mkono wote wanaouliza kwa mshituko na mshangao kana kwamba ni jambo/tukio geni au la ajabu kusikia kuanzishwa kwa chama kipya!
Watu wanaokubali na kuunga mkono mabadiliko/mfumo wa vyama vingi watatia aibu sana kama watachukia kuona chama kipya kinazaliwa, wakati huo wao wakilalama kuwa wanabanwa na chama tawala kisichoruhusu ushindani huru,

Watu hao wanashindwa kumudu ushindani ndani ya mfumo uliopo na badala yake wanatumia mbinu hasi za kuwahadaa wananchi kuwa hakuna chama kingine halali zaidi yao, hii ni dalili ya udictator, umimi, uwao, usisi.

ii) Kuhusu mimi kujua uwepo wa chama kipya cha ACT-Tanzania ni kweli nafahamu uwepo wa chama hiki kipya.
Kuwepo kwa vyama vingi vyenye dira, itikadi na falsafa tofauti ni namna nzuri ya kuweka ushindani huru wa kujiuza kwa falsafa, imani na itikadi zao ili waungwe mkono na umma hatimaye watwae dola,

Dosari kubwa imevikumba vyama vya siasa vilivyopo hivi sasa hapa Tz, waenezi wao wameacha na kusahau kunadi itikadi, falsafa na imani za vyama vyao badala yake wanaeneza shutuma, uzushi na hukumu za matusi dhidi ya vyama vyingine,

Tabia hii imemea na kuota mizizi katika vyama vyote sasa vilivyopo hapa Tz, hakuna hotuba inayoelezea dira ya chama wala fafanuzi ya falsafa yake kwa kuijengea hoja juu ya hali ya jamii iliyopo, wengi huona vyema pale wanapokutana na shutuma ya chama kingine nakuigeuza kuwa hoja zao majukwaani, watu hawa ni watupu kwenye mijadala wanapokutana na mwendesha mjadala au mdahalo anaeweza kushikiria hoja mara nyingi hukuwepa kuhudhuria midahalo na mijadala yenye uchanganuzi wa issues.

Mwisho, NARUDIA MANENO YANGU...''HAKUNA CHAMA CHA SIASA KILICHOANDIKWA KWENYE QURAN WALA KWENYE BIBLIA'' hakuna chama halali wala haramu, vyote lengo lao ni moja tu, kutwaa dola na kuongoza serikali, isipokuwa ubora wa chama au ubovu wake hutokana na utashi wa viongozi wao tu, kuna vyama visivyo na ukabila kwenye katiba zao, lakini utashi wa viongozi wao unajenga taswira hiyo, havina udini lakini utashi wa viongozi wao unajenga taswira hiyo...

ACT-Tanzania itakapoanza ijiweke nje ya siasa za kuwinda matukio na za kutega upepo!!


Nyakarungu Jr 2014
+255-755 023 503


act-agriculture council of tanzania
 
Back
Top Bottom