Kuheshimu taaluma husika

Kuheshimu taaluma husika

Alva

Senior Member
Joined
Dec 1, 2017
Posts
119
Reaction score
127
Habari wana jamvi, kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosema "kuheshimu taaluma husika,
Juzi tumeona mh mbunge Goodluck Mlimba akiomba radhi kwa kushika sindano hali ya kua yeye si daktari au tabibu husika wa fani hiyo, akachutama na watu tumemsamehe kwa moyo mkunjufu kabisa.

Lakini hali hii imezoeleka katika sehemu nyingi tuu, nitatoa kisa kimoja hapa " kuna siku moja jamaa mmoja alipata hitilafu ya umeme katika nyumba yake, akaona amuite fundi umeme aje angamue tatizo ni nini hasa, fundi akataja bei ya kutatua tatizo jamaa akakubali.
Fundi haimchukua mda mrefu kufumbua tatizo la hitilafu ya umeme, hivyo akamuomba jamaa amlipe haki yake kama walivyokubaliana, jamaa akagoma kuona tatizo halikuchukua mda mrefu kutatuliwa kwanini alipe pesa nyingi hivyo , Jamaa akaamua kupunguza kiasi walichokubaliana , fundi kwa shingo upande akapokea...

Fundi alifikiri kwa muda akamuomba jamaa kwamba kuna sehemu hajamaliza vizuri ili umeme usisumbue tena, akapanda juu na kufanya anachojua akaondoka, ilichukua siku 3 tuu umeme haikuwaka tena, jamaa ilibidi afumue mfumo mzima wa umeme asuke upya, gharama juu ya gharama ...

Taaluma ya mtu lazima iheshimiwe, hata huko mtaani hali ni mbaya zaidi, unakuta mtu kajenga Choo lakini ujenzi wa malumalu ni madudu, ili utoe haja ndogo inabidi uwe kama mti ulioegemea nguzo ya umeme huwezi simama wima, kisa tuu alitaka fundi ambaye ni cheap...
Wengine wamebahatika kupata maghorofa huko mtaani lakini ukiingia ndani hizo ngazi kisigino hakienei kabisa, kisa tuu alitaka fundi wa bei rahisi na hakuheshimu taaluma za watu..

Linapokuja suala la taaluma ya mtu tujifunze sana kuheshimu, iwe kilimo, biashara, ujenzi, ufugaji n.k
Nawasilisha
 
me nashangaa watu wanavyowadharau walimu..wanasahau ualimu ndio taaluma mama hapa dunian
 
Back
Top Bottom