iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,927
Huu mradi wa kuhamia dodoma ulianza kuimbwa miaka kadhaa iliyopita lakini haukuwahi kufanikiwa,kimsingi,ulibaki vitabuni tu.
Hatimaye miujiza imetokea,na sasa serikali,kidogo iko dodoma kwa ajili ya Ku satisfy daftari la mahudhurio.
Kinachotokea ni nini?
Waziri,katibu mkuu,naibu katibu mkuu,na baadhi ya wakurugenzi wako dodoma,wataalam wengi waliobaki wako Dar es salaam,hawa watu wanafanyaje kazi bila wataalamu wao.Hapa ndipo posho hunoga,
Mawaziri,katibu wakuu na baadhi ya wakuu wa idara huja Dar es salaam kuhudumia wataalamu waliowaacha,watakaa Dar kama wiki moja, wakila posho zao Nene,baadae hurudi Dodoma,
Wakati huo huo wataalam nao hupishana njiani,huyu anaenda Dodoma yule anarudi kupeleka na kurudisha nyaraka mbali mbali.
Kwa wananchi je? Mwananchi anafika Dodoma ana shida na waziri au katibu mkuu au mkuu wa idara fulani, anajihimu,anapanda basi mpaka Dodoma analala,asubuhi anaamkia wizarani, salaalee!!anaambiwa waziri yuko Dar na atakaa wiki moja,kama unaweza mfate,anapanda basi tena(gharama)anafika Dar anakutana na waziri,waziri anamkabidhi kwa wataalam,wanamhudumia,wakimaliza,wanamwambia hili suala lazima lipitishwe na katibu mkuu,kama unaweza rudi Dodoma....
Upande wa majengo,sasa asilimia zaidi ya 98 ya wizara zote zimepanga majengo(kwenye bajeti ilikuwemo?) Wale maofisa nao waliostahili nyumba wamepangishiwa Dodoma na wameacha Nyumba zao tupu Dar es salaam....kodi inalika.
Sasa kila siku Barua inafika Dar inapelekwa Dodoma ...inarudi Dar....gharama za usafirishaji.
Nadhani haya ni mateso ambayo yatafuatiwa na bajeti ya ujenzi wa majengo ya ghorofa kwa ajili ya wizara huko dodoma kuanzia mwakani wakati pesa hiyo ingefaa kuboresha afya,maji na elimu.
Kiuchumi,hakuna tija kuhamia Dodoma ....kuhamia Dodoma hakuongezi pato la taifa,
Kiusalama kuhamia dodoma hakuna tija ....siku hizi kuna inter continental ballistic missile,mtu kakaa baharini anarusha kombora kigoma.
Kama taifa ....hatujaambiwa eti viongozi wakikaa dodoma ndio tutapata maisha bora.
Kuhamia Dodoma nakufananisha na kujenga Nyumba kwa tofali za barafu!!!