Kuhama Vyama Kumuunga Mkono Mhe. Rais

Kalamu Huru

Member
Dec 2, 2017
11
45
Salamu...!!

Kalamu Huru imepokea taarifa zoeleka kuwa Mbunge wa Kinondoni amejizuru nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya Chama chake CUF na kujiunga na CCM ili kumuunga mkono Mhe. Rais. Huu umekuwa ni mtindo wa kawaida na unazidi kuzoeleka kwa kasi katika saisa ya nchi yetu.

Lakini je, ni lazima kuhama chama ili kumuunga mkono Mhe. Rais? Kalamu Huru inaona hapana. Si lazima. Unaweza kumuunga mkono Mhe. Rais kutokea hapo hapo ulipo na vile vile unaweza kumkosoa kutoka hapo hapo ulipo. Kwa kuwa, hakuna namna kwa mtu mwenye akili sawa sawa akakubaliana na Mhe. Rais kwenye KILA KITU au kupingana naye kwenye KILA KITU.

Kuhama chama kwa sababu tajwa ni kuwakosea wapiga kura wako na pia kukikosea chama chako kilichokuamini na kukupa nafasi hiyo ya kugombea ambayo angeweza kupewa mtu mwingine. Zaidi sana, inaongeza gharama kwa Serikali kwa kurudia uchaguzi badala ya kuelekeza fedha hizo kwenye maeneo ya kipaumbele kwayo mngemuunga zaidi mkono.

Hata hivyo, Kalamu Huru inatambua uhuru wa watu kujiunga au kuachana na chama chochote cha siasa..... ila not to this extent....!!

Na kwa upande wa Upinzani je??? Upinzani unapaswa kukaza nati zote zilizolegea. Upinzani unapaswa kuacha kuendelea kulegeza nati zao hata kama ni ndogo kiasi gani. Jana nilisoma andiko la Malisa G. J, aliloanza kuandika kuwa ameandika na kufuta mara nyingi. Ukilisoma kwa makini hasa ukiyapa maanani yale ambayo yamefutwa katika andiko lile, ni wazi Upinzani wetu unapaswa kuziangalia nati zake moja moja kwa umakini mkubwa na kuzikaza ili mfumo mzima uendelee kutenda sawa sawa.

Ni imani yangu kuwa, upinzani imara wenye mawazo mbadala na media yenye weledi ni muhimu sana kwa Maendeleo ya nchi yoyote.

Pia waweza nifuata Instagram: Kalamu Huru

Alamsiki.

The Quill.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,895
2,000
Mwishowe mafanikio yataangaliwa kwa nafuu ya maisha.
Nyumba bora sio bomoabomoa.
Huduma za Afya, dawa na vifaa tiba. Watumishi wa Afya.
Elimu kwa ubora wa shule msingi hadi Chuo Kikuu. Hapa kuna maslahi ya walimu.
Ongezeko la kipato cha wakulima. Siyo korosho tu. Iende kwenye kahawa, chai, pamba, mahindi nk
Maji safi na salama mijini na vijijini.

Sioni hayo yakifanyika. Flyover zitakuwepo sawa. Labda Bombardier zaidi lakini hao "wanyonge" wataendelea na unyonge wao.
 
Kikinga

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
1,304

Mkosoe uone cha moto
 
Kalamu Huru

Member
Dec 2, 2017
11
45
Mwishowe mafanikio yataangaliwa kwa nafuu ya maisha.
Nyumba bora sio bomoabomoa.
Huduma za Afya, dawa na vifaa tiba. Watumishi wa Afya.
Elimu kwa ubora wa shule msingi hadi Chuo Kikuu. Hapa kuna maslahi ya walimu.
Ongezeko la kipato cha wakulima. Siyo korosho tu. Iende kwenye kahawa, chai, pamba, mahindi nk
Maji safi na salama mijini na vijijini.

Sioni hayo yakifanyika. Flyover zitakuwepo sawa. Labda Bombardier zaidi lakini hao "wanyonge" wataendelea na unyonge wao.
Nachelea kusema, na ukirejea andiko langu la 'Mustakabali wa Upinzani Nchini", kuwa hivyo ni visingizio tu na havina afya kwa upinzani wetu.

Hali ya maisha imekuwa duni daima. Bado walishinda. Dawa zilikuwa hazitoshelezi. Walishinda. Elimu i duni pia. Walishinda. Wameboma Kimara juzi tu. Wameshinda....!!! Kwa nini tujiaminishe hayo hayo yatawafanya washindwe kesho?? Tunajilisha upepo.

Tuache visingizio, get into the game and play to the tune kwa mbinu mbadala zenye kutuhakikishia ushindi.

Hii kulalamika na kujitetea daima kumethibitisha kuwa hakuna manufaa.

The Quill.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom