Kufutwa kwa ada na michango mashuleni

Mish Albert

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
657
581
Habari wakuu

Hivi juzijuzi,serikali ilitoa takribana billion 131.4 katika harakati ya kufanikisha sera ya mheshimiwa rais ya Elimu bure

Pia katika hotuba yake bungeni,waziri mkuu alisema kuwa pesa hizo zitatumika kufidia ada na michango mbalimbali iliyokuwa ikichangishwa kabla

sasa swali langu ni hili,
Ina maana hizo pesa zinafidia na madeni waliokuwa wanadaiwa baadhi ya wanafunzi?

Kwa mfano kuna wanafunzi hawakumalizia ada zao mwaka 2015

Na hawa wanafunzi wa IV ambao hawakulipa ada ya mtihani wa kidato cha nne,
Matokeo yao yatasitishwa mwaka huu mpaka walipe kwanza?Na kwanini?

Msaada wenu ni muhimu wadau!
 
Serilali ilitoa bilioni kama 18 hivi na si hizo aambazo umeziandika. Mengineyo subiri wataalu wake.
 
Hii dhana ya elimu bure naona bado haijakaa sawa.

Kijijini kwetu shule za msingi walikuwa na miradi ya uendeshaji wa shule za chekechea huku walimu wakilipwa na michango ya wazazi. Ikumbukwe walimu wa chekechea hawajaajiriwa na serikali. Baada ya hii dhana ya elimu bure, wale walimu wa chekechea vibarua vimeota mbawa. Watoto wa chekechea wanafundishwa na walimu wa shule za msingi...

Huo ufundishaji sasa ndio kichekesho kikuu.

Uzuri wengine Mungu katuwezesha wanetu wanasoma shule binafsi. Hapa kazi tu!
 
Kwa kuanzia na matokeo ya form two.... Wote waliolipa na ambao hawakulipa hela ya mtihani wote matokeo yametoka. Pia kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo hata kama alikuwa na madeni yameshajifuta.
 
Kwa msaada mdogo tu Ndugu.., usitegemee sana maneno ya wana siasa na khaswa Serikali iliyobobea misongo na mizigo mikubwa kuliko uwezo wake!! just kijimu na ujiwezesheee mambo yako mapema upate kuendelea na mustakabali wa wanao !!
Forget hotuba hewa... Jiendeleze mwenyewe litakapokuja well and good !!
God bless you...
 
Dhana ya elimu bure bado ni kizungumkuti,kuna mambo mengi bado hayajapatiwa majibu kama hayo uliyoyataja mkuu,lakini pia shule nyingi zina madeni mengi ambayo haijulikani yatalipwa vipi.
 
Sahar said:
Kwa kuanzia na matokeo ya form two...Wote waliolipa na ambao hawakulipa hela ya mtihani wote matokeo yametoka
Asante mkuu kwa msaada wako

Ina maana hata hawa wanafunzi wa IV ambao hawakulipa ada,matokeo yao yatatoka pia kama hao wa form II?
 
Back
Top Bottom