Kufungwa kwa flow meter, game changer!

TRUVADA IQ yako ni zero kama huwezi kuutambua mchango wa wapinzani basi wewe bila shaka una mtindio wa akili.
 
Kwa hiyo usalama wa taifa,management ya bandari na top officials walikua hawalijui hili ?

Wanajua ila kwa kuwa ni wanufaika hawakuona umuhimu! Walichosahau ni kwamba, kila lenye mwanzo lina mwisho! Walizani wataendelea na mizaha yao kama desturi! Nami nashauri wote wawajibishwe hadi mkuu wa nchi aliekuwepo wakati husika!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Sijaelewa hapa, kwamba ulitaka wabunge wa upinzani ndo waseme kuhusu flow meter na si suala la Dodoma au?, tokea hilo suala limetokea na akatajwa Waziri kuhusika nini kimetokea baada ya hapo?, nani alihusika na kachukuliwa hatua gani?, umewezaje kumuingiza Zitto alafu ukawaacha mawaziri wenye dhamana na viongozi wengine?,Zitto kama kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo anasimamia pia msimamo wa chama, tunamuunga mkono Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na ufisadi na ACT ndo chama pekee cha upinzani ambacho tokea awali kimekuwa kikimuunga mkono Magufuli kwa juhudi zake, lakini tunalaani hatua zake za kukandamiza Demokrasia, kumbuka kabla hujaenda huko kusema Zitto kuna jambo anakosa, kumbuka amefanya mkutano akaitwa Polisi hiyo kitu haikuwepo katika Utawala uliopita unataka Zitto aweje?, unataka atulie kuona Demokrasia inakanyagwa?, na hata katika hotuba yake, alisema anaona Magufuli atatawala kipindi kimoja kwa sababu Wananchi hawatakubali kunyimwa uhuru wa habari, narudia tena na yeye amekuwa akisema anaunga mkono juhudi za kupambana na ufisadi lakini kitendo chake cha kuminya Demokrasia tutakipinga daima
 
Uandishi Ndo huu tunaotaka nimeipenda bila masharti
 
Flow meter imeshaanza kufanya kazi?
 

HAWAMU=AWAMU....punguza jazba,hata magufuli kuna vitu kavikosa awamu hii ndo mana kawa mtumbua majipu..tumia darubini utaona hasa ndani ya chama chake
 
Swali la msingi la kujiuliza hizo mita zilizofunguliwa zinafanya kazi au ziko katika hali gani. Mana usitake tu sifa ya kuwa umeibua swala la flow meter za bandari wakati. Story yako haijawa na uendelevu baada ya waziri mkuu kutoa maagizo nini kimefanyika na nini hakijafanyika mpaka sasa hivi. Wewe bwana Mwandishi wa Jamuhuri tuletee developing story ya baada sakata zima nini kinaendelea.Ili hizo sifa unazozilazimisha kupewa ziwe na msingi mzima wa habari iliyokamilika
 
Sasa mbona wapinzani waliposema Mkwere dhaifu mliwapinga? Wapinzani wasingeweza kusema kila kitu Mkwere alikuwa na madhaifu mengi hivyo hili la mita lilijumuishwa kwenye kauli moja ya mnyika "Rais Dhaifu" ambayo mliipinga

Mhe Rais mstaafu angekuwa dhaifu tusingefika hapa, kila mtu na zama zake, yeye alikuwa fair mkapiga kelele haya kaja mtendaji tena makelele, mnataka mtu wa namna gani, Zitto yupo vizuri kihoja ila kuna mda huwa simuelewi labda kuna ukweli wa hoja hapa , muda utatuambaa majibu sahihi
 
inaweza kuwa flow meter ndo ilichangia kuwepo kwa petrol stations nyingi kutoka Dar hadi Chalinze. hongera kwa gazeti la jamhuri kwa kuibua ishu hii. yule mama wa wakala wa vipimo namuonea huruma nadhani uhusika wake ni mdogo katika ishu hii ni kama alikuwa anapokea maelekezo tu lazima kutakuwa na mapapa wa ufisadi huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…