Nyakati zinafanana??Suala la currency Ni la Muungano hivyo Kufungiwa Maduka ya kubadikishiwa Fedha Rais wa Znz Hana Cha kufanya wala kuamua Yeye Ni Mpenzi mtazamaji Kama Mimi Na Wewe
Zamani enzi Za Mzee Kambarage ilikuwa ili ubadili Fedha zako lazima upate Kibali Cha Governor
Vijana mliokuwa mnamsoma Kambarage Kwenye Vitabu sasa Na nyinyi onjeni 'asali' tulioishi nayo kwa 23 years
Mkiona nyakati zingine tunamkosoa Mjue tuliumia
Nanyi mtakapokuwa mnaona watu wanasoma Kwenye vitabu kuhusu awamu ya Tano mtakuwa mnakosoa Na vizazi hivyo havitowaelewa
Mtu mweupe umesema sahihi sana, na kiukweli utashangaa sana SMZ wanafuata na kuiga kila kitu kinachofanyika Tanganyika, ila hivi wanavyoiga ni vile vibaya na vyenye kurejesha nyuma waru na nchi kwa ujumla, hawa SMZ hawaigi kujenga miundombinu mizuri na imara wataiga vitu visivyo na macho wala miguu ambavyo haviwahusu ndewe wala sikio.Mimi mpaka hivi sasa linaniuma suala la kufungiwa Bureau de changes hasa hizi za hapa Zanzibar. Bado nina masuali lukuki najiuliza kichwani mwangu ambayo siyapatii majibu.
Kila nikichunguza Zanzibar itanufaika vipi na ufungaji wa hizi Bureaux de change, sipati jawabu. Ina maana leo hii Serikali ya Muungano inataka dola zinazopatikana Zanzibar kutoka sekta ya utalii ambayo kimsingi si ya Muungano wazidhibiti wao kupitia Bureau de change yao ya posta?
Kwa tuliosoma utalii hili ni kinyume na matakwa ya utalii endelevu, na ni kinyume na Sera yetu ya Zanzibar ya Utalii kwa wote. Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzíbar ina Sera nzuri ya Utalii kwa wote, sasa ikiwa mjasiriamali wa Bureaux de change anafungiwa duka lake maana yake yeye hatofaidika tena na mapato ya utalii. Katika hali hii ni sawa na kusema kwamba utalii wa Zanzibar hautomnufaisha tena mfanyabiashara huyu? Sasa je hatuoni kwamba tunapingana na Sera yetu ya utalii kwa wote!
Katika Utalii kuna kitu kinaitwa Tourism Leakage. Wataalamu wanaitafsiri “Leakage” kama ni kitu chochote kinachopelekea mapato ya utalii ya nchi moja kutoka nje ya mfumo wa kiuchumi wa nchi husika. Ni wazi kwamba uchumi si suala la Muungano, hivyo kuifanya Tanzania kuwa na chumi mbili tafauti. Sasa je dola inayopatikana Zanzibar kutokana na utalii sekta ambayo kimsingi si ya muungano ikitolewa nje ya mzunguko wa fedha na uchumi wa Zanzibar itaitwaje kama si Leakage hiyo.
Kwa ufupi, katika takwa moja la utalii endelevu ( sustainable tourism) ni kuajiri jamii inayozunguka utalii wenyewe (surrounding community) ili nayo inufaike na shughuli na mapato ya utalii. Sasa hatuoni kwamba kuzifunga bureau de changes za Zanzibar ambazo kimsingi zinamilikiwa na jamii ya kizanzibari ambao walipaswa kufaidika na utalii wa Zanzibar kwa njia moja ama nyengine na kuifuisha bureau de change ya posta ambayo si milki ya jamii ya Kizanzibari si ni kwenda kinyume na Sera yetu utalii kwa wote tu bali pia ni kwenda kinyume na matakwa ya utalii endelevu? Maana yake dola inayotokana na utalii wa Zanzibar kwa mfumo wa sasa itakwenda kuwanufaisha watu walio nje ya Zanzibar badala ya hawa Wazanzibari walio humu ndani.
Mwisho labda nitowe rai kwa Serikali yetu tunayoipenda ya Zanzíbar na kuitanabahisha kwamba si kila sera inayotungwa na Tanganyika ina maslaha na Zanzibar. Mazingira ya kiuchumi ya Zanzibar ni tafauti sana na mazingira ya kiuchumi ya Bara. Basi ifike wakati kila nchi iwe na sera zake za kifedha ( fiscal and monetary policies) pamoja na kuwa na central banks zake ili kila mmoja apange uchumi wake kwa mazingira ya nchi yake.
Gomesheni kuburuzwa wazenji sio wabara.Mimi mpaka hivi sasa linaniuma suala la kufungiwa Bureau de changes hasa hizi za hapa Zanzibar. Bado nina masuali lukuki najiuliza kichwani mwangu ambayo siyapatii majibu.

Huyu sasa ndiye Pohamba ninayemjua siyo yule aliyedai maji ni anasa.Nyakati hazifanani ila Kinafiki mlikuwa mnalilia Azimio la Arusha lililofutwa Na Wazee wenye busara 1992 Mkawa hamkumbuki hiyo hoja ya 'nyakati'
Sasa limerudi Na Kama mlikuwa mnalililia kinafki Kwenye midahalo Sasa hivi mnakula Matunda ya Kinafki
Msingi wa Azimio la Arusha ilikuwa 'kukata' Mirija ya 'kinyonyaji'
Unaijua Mirija hiyo?
Kama huijui sema nikupe Darsa fupi mujjarab kwa bundle yako ya Mia Tano tu?
Mimi si wa kupewa darsa.Nyakati hazifanani ila Kinafiki mlikuwa mnalilia Azimio la Arusha lililofutwa Na Wazee wenye busara 1992 Mkawa hamkumbuki hiyo hoja ya 'nyakati'
Sasa limerudi Na Kama mlikuwa mnalililia kinafki Kwenye midahalo Sasa hivi mnakula Matunda ya Kinafki
Msingi wa Azimio la Arusha ilikuwa 'kukata' Mirija ya 'kinyonyaji'
Unaijua Mirija hiyo?
Kama huijui sema nikupe Darsa fupi mujjarab kwa bundle yako ya Mia Tano tu?
Kwani benki huko Zanzibar hawabidilishi fedha?

Hivi exchange rate ya huko na huku huwa ziko sawa?
Kama ni tofauti basi kila mtu ale anavyotaka
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Hivi hujuwi kuwa Zanzibar ni kimkoa chetu? Kwani huko Zanzibar mna sarafu yenu ya pekee?
Mtafata tunayoyataka sisi mkitaka msitake. Mapinduzi daima.