Kufungia magazeti si dawa ya kuwaziba midomo watnzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungia magazeti si dawa ya kuwaziba midomo watnzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Aug 3, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Watanzania wamekuwa kiakili na kimtazamo kuliko kipindi chochote kile toka enzi za kudai uhuru wa Tanganyika.Ahitaji elimu ya chuo kikuu kutambua nchi yetu inatafunwa na mwenye meno.Ahitaji akili ya ziada kujua kuwa wachache wana jineemesha kwa kutumia dhamana ya madaraka tuliyo wapatia.

  Nasema hivyo kuzingatia hali inayo likumba taifa letu,ukomo wa kufikiri na kuongoza wananchi hatimaye sasa umefika mwisho.Firauni alipoambiwa amezaliwa mfalme atakaye kuwa mtawala wa Misri alichanganyikiwa kiasi cha kutoa amri ya kuua watoto wote wa kiume waliozaliwa ili aweze kulinda madaraka yake na kuhifadhi tamaa yake ya kujilimbikizia madaraka pamoja na mali,lakini mwisho wa siku kilichokusudiwa na Mungu kilitekelezwa.

  Kitendo cha serikali kufungia magazeti ni udikitekta ambao hauwezi kuvumilika katika kipindi hiki ambacho magazeti ndiyo yamekuwa mtetezi mkubwa wa haki za wanyonge.Leo nani ana bisha kuwa bila magazeti hali iliyoko hivi sasa ingekuwa zaidi ya ilivyo sasa.

  Mpaka lini serikali itaendelea kukikimbia kivuli chake kwa staili zisizo na mashiko,lengo hasa la serikali kulifungia gazeti hili la Mwanahalisi si tu kuwa kumeidhalilisha serikali bali pia ina wazidishia chuki wananchi na kutokuwa na imani na serikali yao.Kitendo kilichofanywa na waziri mwenye dhamana hiyo kina zidisha doa ambalo sabuni ya kuliondoa doa hilo itaigharimu serikali.


  Hali hii imeni fehedhesha sana na inabidi kulaaniwa na wapenda demokrasia wote nchini bila kujali itikadi za kivyama.Nakumbukua Waziri mkuu wa zamani wa awamu ya tatu wakati wa mchakato wa kupitisha majina yatakayo toa mgombea urais kupitia CCM alisema"Ni hatari sana kwa kiongozi au mtu anayetaka uongozi kununua vyombo vya habari kwa lengo la kuwachafua wagombe wenzake,ni hatari sana akikamata madaraka ana weza kutumia mtutu wa bunduki katika kuwa buruza wananchi"

  Haijapita hata muongo mmoja,yule yule aliye yatumia magazeti yale yale ana tumia nguvu ya ziada kuyafungia kwa kuwa tu yamekuwa tishio kwa kuanika yale ambayo wananchi wanapaswa kuyajua.Tumeona sheria kandamizi ya kuvidhiti vyombo vya habari ya miaka ya sabini leo inaendelea kutumika bila kujali kama ina endana na wakati husika.

  Na shauri kwa kupitia bunge letu tukufu sirikali ilete muswaada wa kufutilia mbali mhimili wa mahakama kwa kuwa tu kwasasa hauna kazi na kazi yake inafanywa na serikali,kuliko kuwalipa watendaji wa mhimili huu ilihali serikali ina uwezo wa kuwa refari,mchezaji na mshangiliaji kwa wakati mmoja.

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe,kuna haja gani basi ya kujinasibu kuwa utawala huu una thamini mchango wa media kwa kuweza kuwaelimisha wananchi ilihali haki hiyo na mchango huo wa media una nyakuliwa kwa kutumia mkono mwingine.

  Watanzania watabaki kuwa Watanzania, vyama na uroho wa madaraka vitapita na midomo ya Watanzania itaendelea kufunguka,kwani kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

  Leo serikali imethubutu kulifungia gazeti la Mwanahalisi lakini ikae ikikumbuka kuwa jela ya mwanahalisi imo ndani ya mioyo ya Watanzania na kamwe hataisahaulika.Ndo maana bado naamini kuwa sikio la kufa siku zote huwa halisiki dawa na mfa maji heshi kutapatapa
   
Loading...