Kufunga barabara/mtaa katika Jiji la DSM


D

Duterte

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2016
Messages
1,066
Likes
1,106
Points
280
D

Duterte

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2016
1,066 1,106 280
Wasalaam wanaJF,
Rejea kwenye kichwa cha habari husika. Kuna tabia zinaendelea kushamiri katika Mji wetu wa DSM za kufunga barabara au mitaa bila kufuata taratibu na kujali watumiaji wa njia hizo.

Hapa nitatolea mfano wa njia ambazo zimekuwa zikileta usumbufu kwa wakazi au Watu wanaofanya shughuli zao katika eneo husika.

Kuna hii sehemu maeneo ya Jamatini (Upanga), katikati ya barabara ya Ali H. Mwinyi na Aly Khan ukiishia Mtaa wa Nkomo (unatokea mataa ya Agha Khan).

Kuna maghorofa ya makazi hapo, zamani kulikuwa na njia takribani 6 ambazo zilikuwezesha ukiwa unatokea Malik Rd (Diamond Jubilee) ukikata kushoto Aly Khan Rd unaweza kutumia hizo njia fupi (short cuts) kuingia Ali H. Mwinyi bila kuzunguka mpaka makutano ya hizo barabara mbili tajwa.

Hao wakazi kwenye hayo maghorofa wamejichukulia maamuzi ya kuweka mageti na kuziba hizo njia.

Swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku nikipita maeneo yale, Je ni nani aliyeruhusu njia zile Kufungwa!!

Mbali kwa wanaotumia vyombo vya moto, waenda kwa miguu wanapata shida ya kuzunguka mbali.

Naomba tuzitaje na sehemu au maeneo mengine ambayo yana karaha Kama hizi.

Nawasilisha hoja.

Duterte.
 

Forum statistics

Threads 1,274,335
Members 490,676
Posts 30,508,696