Tatizo la Watanzania ni kuongea bila kufanya utafiti, sera ya elimu yetu ndo tatizo, tendo la ujifunzaji ni rahisi kwa mtoto mdogo maana hana vitu vingi kichwani mwake, ninachotaka kukisema hapa ni kwamba kiingereza kingeanzwa kufundishwa toka chekechea tena lingekuwa soma kipaumbele na kufundishwa na walimu wenye weredi mkubwa.
MADHAIFU YA ELIMU YA TANZANIA NI.
1. Chekechea,, shule nyingi za serikali hazina madarasa ya Chekechea hivyo asilimia kubwa ya watoto wadogo wanafundishwa kwenye vituo vya watu binafsi tena kwenye mazingira yasiyo rafiki kwa watoto na bila uangalizi wowote. Ukianza vibaya usitegemee kumaliza VIZURI
2. Uelewa wa Watanzania kuhusu umuhimu wa kitu ELIMU ni mdogo sana, mpaka sasa hawajui nani ni mchawi wa ELIMU ya watoto wao kuwa ni serikali ndo maana hata serikali yenyewe baada ya kuona haijagunduliwa haioni umuhimu wa kuboresha elimu husika.
3. Viongozi wa serikali hawapo tayari kuboresha elimu maana watoto wao hawasomi kwenye hizo shule za serikali, hivyo hawaoni umuhimu wa kuboresha elimu husika.
4. Wanafunzi,,,, Watoto wetu hatujawajenga kujitambua na kuthamini kile wanachokifanya.
5. Jamii inayowazunguka hawa watoto /wanafunzi nayo ni tatizo maana inawarubuni hawa watoto kwa kufanya nao mapenzi na hata kuwapa MIMBA.
6. Miundombinu ya shule kwa ujumla sio rafiki kumfanya mtoto avutiwe nayo. Watalaam wa elimu wanasema mazingira mazuri ni factor muhimu kwenye ujifunzaji sasa nenda kwenye SHULE ZA SERIKALI madarasa yamekuwa MAGOFU utadhani mabanda ya kufugia KUKU na SUNGURA kuna watu watadai zamani walisomea madarasa kama hayo na walifaulu, dunia ya sasa haiko kama zamani.
7. Siasa kuingia kwenye Elimu kitu kinachopelekea walimu ambao ndo wasimamizi wa wanafunzi kutokuwa na moyo wa kuwafuatilia wanafunzi watukutu kwa kuhofia usumbufu usio na maana.
8. Uwekezaji mdogo kwenye Elimu,,, Nimeambiwa kwamba na ni uhakika kwamba serikali toka mwaka Jana au mwaka juzi ilivyokusanya vitabu baada ya kugundulika vina makosa mpaka sasa hawajasambaza vitabu mashuleni hivyo kupelekea kuzorotesha elimu.
Sababu zipo nyingi sana leo ngoja niishie hapa