KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,896
- 36,213
Habari za jumapili wapendwa.......
Bila ya shaka sisi sote Mungu ametujaalia uzima na afya tele.....na wenzetu wengine waliopo kwenye mitihani ya magonjwa Mungu awaponye warudi kama zamani na kuyafurahia maisha..........
Bila ya kupoteza muda ningependa leo kushirikiana nanyi suala hili ambalo kwa namna moja au nyingine limekuwa likibomoa au kuleta migogoro kwenye mahusiano mengi na kwenye ndoa nyingi.......
Kufukua MAKABURI maana yake ni kuchungulia mambo ya zamani ya mpenzi wako.......kama ilivyo tasfiri ya neno KABURI maana yake ndani yake kuna kumbu kumbu mbaya......ambazo kwa namna moja au nyingine tusingependa zitujie kwenye akili zetu............makaburi yamefukia wapendwa wetu ambao hatungependa kuwapoteza.......
Kama ilivyo kwenye mahusiano kuna kumbu kumbu ambazo kwa hali yoyote hatungependa ziturudie akilini mwetu kwani zimebeba taarifa na picha mbaya......lakini maisha yanaendelea kwa kuwa tumeamua kuyafukia na kuyasahau........
Maisha ya mwanadamu hadi kufikia sehemu alipo yamebeba historia na kumbu kumbu nzuri na mbaya. Kuna watu kwenye historia zao walibakwa na watu waliokuwa wakiwaamini....kuna watu wana historia mbaya kwenye mahusiano ya nyuma kiasi kwamba waliapa kuwa hawatapenda tena
Kuna watu walishaamini kuwa hawatakuja kuwapata wenza sahihi maishani mwao.....hivyo basi watu wameamua kuwa na tabasamu kwenye nyuso zao kwa kuwa wameamua kuzifukia kumbu kumbu hizo na kuanza mwanzo mpya...........
Tunapoanzisha mahusiano maana yake tumekutana watu wawili wenye historia na kumbu kumbu tofauti tofauti zikiwamo mbaya na nzuri..........
Ili mahusiano yastawi na kudumu yanatakiwa yawe na mwanzo imara.......mwanzo imara daima hauwezi kuwa imara kama bado unaingia kwenye mahusiano hali ya kuwa bado una kumbu kumbu ya mambo yako ya zamani.......
Wengine hata hufikia hatua ya kuwahukumu wapenzi wao wapya kutokana na kumbu kumbu zao za zamani.........
Faida na busara pekee ya kumbu kumbu za nyuma ni kujifunza kulingana na makosa yako ili usije ukafanya makosa kama yale yaliyosababisha ukawa na kumbu kumbu mbaya au kuvunja mahusiano yako.......na hvyo mwanadamu mwenye akili timamu anavyofanya.........
Tukiwa na wapenzi wetu wapya tusipende kufukua fukua mambo ya zamani kwani kumbukumbu hizo wakati mwingine tukiambiwa zinaweza kukaa akilini mwetu na kutuondolea utulivu........kuwa na amani acha mambo yaendee.........
Cha msingi ni kukaa na mpenzi wako mpya kuangalia namna ya kuuanza mwanzo mpya wa safari yenu ya kimapenzi na kumuomba Mungu awaongoze vyema katika hilo ili mzishinde changamoto na mitihani yote ya mbele.......
Bado nasisitiza kuwa hakuna faida ya kufukua makaburi zaidi ya kujifunza kulingana na makosa.....na hayo ni majukumu ya mwenye kumbu kumbu hizo ili kujisahihisha.......
Nawasilisha.......