Ndugu yangu LEE VAN CLEEF usiumize sana kichwa !!
Kuna aina nyingi ya mbwa ila kama unahitaji mbwa kwa ajili ya ulinzi basi nakushauri tafuta hata hii mbegu ya kienyeji,awe ni dume ,kisha unamuhashi,kama hapo unapoishi kuna bucha jirani,ongea na mtu wa buchani kila siku awe anakukusanyia ile mifupa midogo midogo kisha unamchemshia, unachanganya na chakula cha dukani kinaitwa '' DOG SPECIAL DIETY''.
Baada ya miezi kadhaa utaniambia, ila kuna dondoo kadhaa za kumtunza mbwa ili awe mkali mfano
1. Mbwa anakula mara moja tu kwa siku,mfano mimi wa kwangu ni saa mbili usiku hadi saa mbili usiku, chakula na maji ya kutosha.
2.Mbwa mwiko kuona watu ovyo yaani anatakiwa kukaa kwenye banda mda wote isipokuwa usiku tu.
3.Zingatia sana dawa kama vile za minyoo,viroboto,kupe nk pia bila kusahau chanjo ya kichaa cha mbwa !!
NB,hizi njia ni kwa mujibu wangu mwenyewe wajuzi fungukeni zaidi tuelimishane !!