Duh kwa hii topic ni tamu sana. Mimi huwa nakomaa kwenda hizo shopping lakini inataka moyo. Kwa masela wengi wetu ukienda shopping unajua kabisa unataka jeans moja na t shirt labda unachukua biashara imeisha. Sasa huu ubavu wa kushoto bwana mkifika anataka sidiria mbili,atachagua arobaini,ajaribishe kumi na tatu,ili achukue mbili. Hapo inabidi mlume inabidi ukomae tu,hapo bado hamjaingia maduka kadhaa ambayo hanunui kitu,na akifika kwenye yale maduka ya vitu vya kinamama ndo nahisi yaani tumakaa humo masaa zaidi ya matatu. Sidhani hata kama huwa anahisi njaa wakati wa shopping,mbaya zaidi una mahesabu ya gemu la man united na liverpool linaloanza saa saba unusu ( kwa saa za nilipo). Hapo inabidi ukomae na kumuharakisha huwezi wala hutaki na wala huna ubavu maan usiku unakuja,utanuniwa mpaka ushangae. Kweli utu uzima dawa.