Kufanya harusi bila Send Off ni sawa au haipendezi?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,810
Habari wadau,

Mimi na mchumba wangu tumepanga kufanya harusi yetu mwezi wa nne mwishoni, plan yetu ni kwamba tutafunga harusi peke yake lakini hakutokuwa na send off. Tumeamua hivyo kwasababu tumeona hamna umuhimu wa kuweka send off ya milioni ishirini na harusi milioni ishirini wakati huo huo bado sijui kitchen party.

Tumeamua hivyo kwa mapenzi yetu wenyewe lakini wakwe wangu hawataki wanaona kwamba kutofanyika kwa send off ni kama aibu kwao.

Binafsi sipo tayari kufanya hizo shughuli zote kwasababu za kiuchumi nahitaji harusi pekee. Hivyo imekuwa mvutano huo baina yangu na wakwe.

Mawazo yenu wakuu
 
mmh hata ingekuwa ni mimi kwa hadhi ya wazazi wangu lazima ningefanya sendoff harusi tunakusanya ndugu wa mume 20 na upande wangu 20 basi ...ningekushauri harusi yenu iwe simple tu... ila kuagwa lazima binti aagwe..
 
em nisadie.... sasa huyu hapa anakuwa anahusika vp hapo wakati wao ni waalikwa.. maamuzi ya mwisho ya kufanya send off si wanayo wakwe wenyewe.. au mi ndo cjaelewa?
 
inaonekana hana nguo nzuri ya kuvaaa siku hiyo..halafu mfuko wake haujatuna vizur ..anawaza..hajui kwamba yeye amealikwa hatachangia chochote..
 
Kwani send off inakuhusu vipi mkuu!! Huo ni mzigo wao waachie wenyewe, we komaa na linalokuhusu(harusi)
 
mm nimeoa mwaka jana mwezi wa kumi na moja, nimegundua wengi wetu tunauoga wa maisha. Kama huo ulioonesha wewe, toka lini send off na kitchen party ukahusika mwanaume???, gharama hazikuhusu. hasipofanyiwa pia inamaana hajaagwa kwao.
 
Send off ni ya upande wa mwanamke so kila kitu kwa maana ya maandalizi yake kitahusu upande wa mwanamke na upande wa kiume wanakua kama waalikwa tu.Na harusi inahusu mwanaume na upande wa kike ni waalikwa tu
 
send off si inamhusu binti??? sasa wazee wa binti si wafanye hyo sherehe kwani we unahusika vipi hapo?? kwani unatakiwa kughramia hyo send off au kitchen party kwa minajili ipi?? waambie nyie fanyeni kama mntaka.. chaaaaa!!!

Na huu ndio ukweli send of gharama yako ni kuhudhuria tu
 
Back
Top Bottom