chiefnyumbanitu
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 906
- 426

Wafanyabiashara hao ambao walikutwa wakizikusanya simu hizo katika maduka mbalimbali yanayouza simu kariakoo wamesema kuwa soko la simu hizo sasa limehamia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Msumbiji na visiwani vya Comoro.
Akizungumza na Zama Mpya jana ikiwa nimasaa machache baada ya TCRA kuanza kutekeleza mpango wake wa kuziondoa simu zisizokuwa na viwango katika soko hapa nchini, mfanyabiashara Hamisi Selemeni alisema ameamua kupita katika maduka kununua simu hizo na kuzipeleka nchi nyingine kwa lengo la kujipatia riziki kwavile haziwezi tena kufanyakazi hapa nchini.
Naye mmiliki wa duka la simu Juma Saidi ameelezea kusikitishwa kwake na utaratibu huo wa TCRA ambao amedai haueleweki licha ya kuanza kutumia mtambo unaidaiwa kutambua simu origino tu, simu zisizokuwa na IMEI bado zinatumika na kudai kitendo hicho kinawapa wakati mgumu wauzaji wa simu na kinaweza kuwaketea migogoro na wateja wao.
Hawa TCRA sijui vipi ni jana tu wameanza utaratibu huu mpya lakini leo simu feki ukiitumia inafanya kazi kama kawaida wanatuweka katika wakati mgumu kibiashara hasa ukizingatia tangu watangaze kuziondoa simu feki sokoni biashara imekuwa hakuna kabisa, nilitarajia jana wakimaliza zoezi lao wananchi watarudisha imani lakini kwa utaratibu huu sijui alisema.
Ikiwa ni siku ya kwanza tangu kuanza kwa zoezi hilo TCRA wametangaza kuzizima simu laki sita na elfu thelathini ambapo wamedai kuwa asilimia 2.6 ya simu zote zilizopo nchini ni feki.
Tangu mamlaka hiyo ya mawadiliano itangaze tarehe ya usitishwaji wa matumizi ya simu feki hapa nchini, wananchi wamekuwa wakilalamikia kutotolewa kwa elimu ya kutosha juu ya utaratibu huo kitendo ambacho kulikuwa kikiwapa wakati mgumu kwa kutoekewa nini cha kufanya.
Uchunguzi uliofanywa na Zama Mpya juni 16 mwaka huu siku ambayo ilikuwa ya kuanza kwa zoezi la uzimaji wa simu feki majira ya saa sita usiku wananchi wengi hawakulala walikuwa wakisubiri kuona hatma ya simu zao.
Wakati huo huo kuna taarifa kuwa baadhi ya watu wajanja wameshatafuta mbinu ya kuulaghai mtambo huo kwa kutumia njia za kimtandao ambapo namba zao zenye kutambulisha ‘line’ za simu mbalimbali (IMEI) zinaweza kubadilishwa kwa hatua chache tu na kufanya mtambo huo kuzisoma namba hizo kuwa ni za halali.