Kuenjoy trip ya Tarangire na serengeti

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,153
2,646
Nina plan ya kwenda kufanya utalii wa ndani, na sehemu nilizojipangia kwenda ni mbili tu ambazo ni Tarangire na Serengeti na kote huko sijawahi kufika katika maisha yangu, kwa sasa nipo Dar na nategemea kupata likizo mwezi May, kwa wazoefu natakiwa kuwa na estimation budget ya kiasi gani ili niweze kuenjoy utalii wa ndani maeneo hayo niliyoyataja?

Nitashukuru sana kwa maelezo ya kujitosheleza.

Mungu awabariki
 
ukifika arusha Kuna ofisi nyingi za tour operators watakupa options nyingi pamoja na bei sawa hapo mwenyewe ndo utaamua, ila jaribu kupita ofisi zaidi ya 3 au zaidi ujiridhishe kwanza
 
Nakushauri u-replan upya iyo tripp yako alafu fika maeneo husika kujua mchakato mzima ndipo uje mzee...
 
Nadhani unaweza kupitia Manyara ukitoka Tarangire halafu unachepuka Ngorongoro ni mbuga zilikaribu karibu sana budget ikiwa kubwa nenda Serengeti.

Kama una gari 4W ni bora kuendesha gari mwenyewe utapunguza gharama kubwa sana.
 
Nina plan ya kwenda kufanya utalii wa ndani, na sehemu nilizojipangia kwenda ni mbili tu ambazo ni Tarangire na Serengeti na kote huko sijawahi kufika katika maisha yangu, kwa sasa nipo Dar na nategemea kupata likizo mwezi May, kwa wazoefu natakiwa kuwa na estimation budget ya kiasi gani ili niweze kuenjoy utalii wa ndani maeneo hayo niliyoyataja?

Nitashukuru sana kwa maelezo ya kujitosheleza.

Mungu awabariki
Nenda hadi Arusha pale kuna ofisi za TANAPA huwa kuna siku wanakuwa na basi ambalo huenda mbunga ya Tarangire likiwa na wanaoenda kutalii ,kwa siku hizi sijui bei zao lakini kipindiilikuwa 25000 kwenda na kurudi,lakini ukienda kwa hawa tours kwa package ya watu 4 huanzia USD 400 kwa siku 2,kukodi gari ni USD 200 kwa siku lakini hapo kila kitu unajitegemea,huo ndio ufahamu wangu na kama Serengeti kwanini usipitie Musoma,kwa maana Serengeti ipo wilaya ya Serengeti unaanza kuburudika na wanyama kuanzia pale kwenye daraja la kati ya Lamadi na Bunda
 
serengeti pako poa hasa kama una usafiri binafsi waweza fanya day trip na kulala Mugumu nje ya mbuga, hyo itapunguza gharama za malazi na chakula ndani ya mbuga.
 
ukifika arusha nitafute mm ni tour guide uko mwenye au na siku ngapi utahitaji kutalii katika mbuga izo au nitafute kwa 0719309585
 
Nina plan ya kwenda kufanya utalii wa ndani, na sehemu nilizojipangia kwenda ni mbili tu ambazo ni Tarangire na Serengeti na kote huko sijawahi kufika katika maisha yangu, kwa sasa nipo Dar na nategemea kupata likizo mwezi May, kwa wazoefu natakiwa kuwa na estimation budget ya kiasi gani ili niweze kuenjoy utalii wa ndani maeneo hayo niliyoyataja?

Nitashukuru sana kwa maelezo ya kujitosheleza.

Mungu awabariki
Mkuu kwa habari ya utalii lazima uwe wazi ktk aina ya usafiri unao utaka kuutumia. Ili kfurahia safari ya utalii unatakiwa aidha utafute kundi la kuungana nalo (joining safari) ambapo mtachangia gharama ya usafiri na tipu ya wahudumu wenu hasa dereva napishi endapo mtakuwa naye, mfano mkiwa watalii 6 na gharama ya safari kwa siku ni dollar 200, mtaichangia wote hivyo kukupa unafuu wa gharama au endapo utaamua kugharamia safari wewe peke yako au na familia yako utalazimika kulipia dollar kati ya 200 nakuendelea bila kusahau malazi ni juu yako aidha hotelini au kambini kulala kwenye hema la kawaida au la kifahari (luxury tent)
 
ukifika arusha Kuna ofisi nyingi za tour operators watakupa options nyingi pamoja na bei sawa hapo mwenyewe ndo utaamua, ila jaribu kupita ofisi zaidi ya 3 au zaidi ujiridhishe kwanza
Shukrani sana kiongozi kwa ushauri!
 
Back
Top Bottom