Wadau kuna jambo linaniumiza akili sana,
Kuna mdada nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa, pamoja na mapungufu aliyonayo (hasa kuwa na mtoto na mwanaume mwingine) niliamua kuwa naye maana hata mimi nina mapungufu yangu pia!
Sasa kilichonifanya niandike hii mada ni kitendo chake cha kutotaka kupata mtoto, hili amekuwa akiniambia waziwazi kwamba mpaka mtoto wake afikishe 10 years, na katika kuthibitisha hili kama mwezi mmoja uliopita alipata ujauzito.
Aliniambia huku akinipa story za kwamba eti ameongea na daktari na kamwambia kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto mlemavu, hivyo kaamua kutoa mimba! Nilijaribu kumdadisi ni dawa gani kamywa alishindwa kunambia.
Mimi sikuwa na neno ila sikukubaliana naye hata kidogo, ye mwenyewe baadaye akaonesha kutokuwa na msimamo..mara nataka nizae kesho yake tena anabadirika! Baadaye baada ya kumbana akanambia kwamba pamoja na daktari kumwambia hivyo, pia yeye haitaji mtoto!
Kiukweli roho imeniuma, maana hapa nilipo kanipa taharifa tu eti mimba kashaitoa, siyo siri sina hamu naye hata kidogo na mapenzi kwake ni kama yanasoma negative!
Mliowahi kutana na hii hali, hivi inawezekana kuendelea kumpenda mwanamke baada ya kutoa mimba!?