Kuelekea ushirikiano wa kikanda ktk Vyuo vikuu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea ushirikiano wa kikanda ktk Vyuo vikuu...

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Gurta, Apr 21, 2012.

 1. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nimetembelea watani wetu katikati ya wiki hii inakwisha, na nikabahatika kutembelea chuo kikuu kimoja cha binafsi kilichopo nje kidogo ya Nairobi. Na hapo nakutana na uzinduzi wa taasisi (idara) maalum itakayo kuwa na jukumu la kushughulika na masuala yanayohusiana na "ushirikiano wa kikanda wa Afrika Mashariki" au kwa kimombo Regional Integration.

  Sina uzoefu na vyuo vya Tanzania lakini upekuzi wangu kidogo niliofanya kwenye tovuti za baadhi ya vyuo ikiwamo UDSM na UDOM na nimeshindwa kuona jitihada za taasisi hizi za elimu ya juu katika kulichukulia suala la ushirikano wa Afrika Mashariki kwa uzito unaostahili. Je, kuna chuo kikuu chochote nchini chenye programu/taasisi/idara/kituo maalum kwa ajili kushughulikia masuala yahusianayo na shirikisho la Afrika Mashariki na changamaoto zake?

  Endapo tuna nia ya kuwa na ushirikiano wa kiuchumi, ki-forodha na hata ndoto za shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki;
  • Je, ni kwa namna gani taasisi za elimu ya juu nchini hapa zinafanyia kazi suala hili hasa katika kuwaandaa vijana wasomi kwa changamoto hizo na kuwapa nyenzo za kuingia katika soko hilo lenye ushindani?
  • Nini kifanyike?
  • Tumechelewa? Na kama ndio tunasubiri nini?
  • Je, kunahitajika intervention ya serikali kuu kuhimiza taasisi hizi kuanzisha idara maalum za kushughulika na masuala ya Ushiriakino wa kikanda?
  Natambua nafasi ya siasa, lakini hebu tuiweke kando na kujadili kitaaluma zaidi. Karibuni...
   
Loading...