Kuelekea UEFA champions league final

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,584
Kuelekea UEFA champions league final

NOTE:

Mwaka 1998..Mjini Amsterdam,nchini Uholanzi ilipigwa Finali ya kibabe ya UEFA ya JUVENTUS v REAL MADRID.Mechi ilikuwa ngumu na yenye upinzan,lakin Goli la Bwana PEDRAG MIJATOVIC kweny kipind cha pili akipiga shuti kali na mguu wake wa kushoto iliwashuhudia Juventus wakirudi mikono mitupu Italy......Swali la kujiuliza Real Madrid ataendeleza ubabe au Juve atalipa kisasi ??

download.php

Madrid vs Juventus bonge la game pale UK.itakuwa fainali ngumu kweli..maana juventus itahitaji kulichukua taji ambalo waliporwa na barca 2015 na Madrid watahitaji kuweka rekodi ya kuchukua mara mbili mfululizo…

Juventus-vs-Real-Madrid.jpg

Juventus lazima watakuja na mbinu yao ya kujilinda muda mwingi wa mchezo huku mashambulizi yao yakiwategemea Mandzukic,Dybala na Higuain pia hata Cuadrado,naamini wataanza na mabeki wakati watatu (BBC) na midfielder wawili Khedira na Pjanic(ingawaje siku za karibuni wamekuwa wakipenda kutumia mabeki wawili wakati ).Kwa mfumo wa mabeki watatu wakati utawapa Real Madrid wakati mgumu sana kupata nafasi kwenye final third ya juve.Mfumo huu ni rahisi kwa juventus kuwazuia Madrid ukizingatia real marid wamekuwa wakiwatumia sana Marcelo na carvajal kuleta mipira ya cross kwa benzema na ronaldO.Pia ili kuwazuia madrid ni lazma kumnyima nafasi huyu goal scoring machine(Ronaldo),yote hii itategemea juventus kaba wataweza kushina battle la midfield..kwenye kushambulia juventus wamekuwa wakimtumia Paulo Dybala kama mtu wa kutafsiri mashambulizi yao,dybala anazunguka uwanja mzima,Dybala anafunga na ku assist,huyu ndio key player wa Juventus.
Prediksi-Skor-Juventus-vs-Real-Madrid-4-Juni-2017.jpg

Zidane atakuja na mbinu zake zile zile za kihuni kwenye game kubwa…cha kwanza huwa anajilinda na kushambulia kwa kushtukiza huku akitegemea speed ya Ronaldo benzema na winger mwingine ambaye anaweza kuwa Bale ,Isco,Rodriguez au Asensio...defense ya Madrid itaunganishwa na Casemiro ambaye yuko ki ulinzi zaidi ukilinganisha na Krose na Modric ambapo wao kazi yao ni kufanya Real Madrid inakuwa na mpira na kusambaza mipi haswa kwa Marcelo na carvajaal..

Eneo la kiungo ndilo litakalo amua hiyo game,aamini vita kali itakuwa kwenye kiungo.kwa Juventus watakuwa na kazi ya kuwazuia Kroos na Modric wasiweze kupiga pasi ambazo zitawafikia Marcelo na Carvajaal.

Kwa upande wa ulinzi real Madrid wana tatizo kiasi…goalkeeper K.navas amekuwa na makosa madogo madogo…pia wamekuwa wakiandamwa na majeraha haswa pepe,varane na Marcelo ambayo imepelekeaa Nacho Fernandez kupata nafasi ya kucheza msimu huu Ni wazi kuwa game itakuwa ya nguvu na kasi huku real Madrid wakitawala mchezo na juventus watajilinda na kushambulia kwa kushtukiza…

Ronaldo na Dybala ndio watu ambao nategemea wataamua mechi ingawaje kwenye mechi kama hizi ingawaje mchezaji huwa yeyote anaweza kuamua mechi.. Pia kwenye hii game nadhani ndipo mahali ambapo buffon na ronaldo wanatakiwa kutuonyesha nani kati yao anastahili tuzo ya mchezaji bora wa dunia japo ronaldo ana nafasi nyingine ya kuonesha uwezo wake kwenye kombe la mabara mwezi june nchini Russia

Juve wanakumbukumbu ya mwaka 1998-5-20 walipofungwa na Madrid 1-0

Katika fainali ile ambayo Juve ilipoteza ilikuwa na Zidane(Mchezaji wa Juve katika fainali ile) na kikosi kilikuwa kama ifuatavyo

upload_2017-6-1_1-25-25.png

Baada ya kukutana mwaka 1998 watakutana tena Katika fainali ya jumamosi hii ambapo mchezaji wa Juve wakati huko Zidane akiwa upande wa pili wa shilingi

Timu yeyote inaweza kupata ushindi katika fainali hii hivo tungojee tuone uhondo huu kutoka Cardiff,Wales

Pitia na hii record

Mwaka 1998 fainali champions league
Madrid 1-juventus 0

Mwaka 2003 nusu fainali
Madrid 2- juve 1
Juve 3- madrid 1 (madrid wakatolewa)

Mwaka 2005 hatua ya 16 bora
Madrid 1- juve o
Juve 2-madrid 0 (madrid wakatolewa)

Mwaka 2009 hatua ya makundi
Juve 2- madrid 1
Madrid 0- juve 2

Mwaka 2014 hatua ya makundi
Madrid 2- juve 1
Juve 2- madrid 2

Mwaka 2017 fainali
Madrid..... - juve .....

Ikumbukwe hakuna timu iliyobeba hili kombe mara 2 mfululizo,pia records zimewekwa ili zivunjwe.Ugumu wa mechi unakuja pale ambapo Lile jopo la wahuni pale nyuma la wataliano wa Juventus hawajawahi kulibeba hili kombe,pia Cristiano Ronaldo anahitaji kulibeba akabebe Ballon'dor yake ya 5 ili ubishani upungue mitaani

Usitume wavulana katika shughuli za wanaume

Mimi Deadbody Nipo Juventus na naona fainali hii Juventus 1 VS Madrid 0

FT (1-0)
 
Kuelekea UEFA champions league final

download.php

Madrid vs Juventus bonge la game pale UK.itakuwa fainali ngumu kweli..maana juventus itahitaji kulichukua taji ambalo waliporwa na barca 2015 na Madrid watahitaji kuweka rekodi ya kuchukua mara mbili mfululizo…

Juventus-vs-Real-Madrid.jpg

Juventus lazima watakuja na mbinu yao ya kujilinda muda mwingi wa mchezo huku mashambulizi yao yakiwategemea Mandzukic,Dybala na Higuain pia hata Cuadrado,naamini wataanza na mabeki wakati watatu (BBC) na midfielder wawili Khedira na Pjanic(ingawaje siku za karibuni wamekuwa wakipenda kutumia mabeki wawili wakati ).Kwa mfumo wa mabeki watatu wakati utawapa Real Madrid wakati mgumu sana kupata nafasi kwenye final third ya juve.Mfumo huu ni rahisi kwa juventus kuwazuia Madrid ukizingatia real marid wamekuwa wakiwatumia sana Marcelo na carvajal kuleta mipira ya cross kwa benzema na ronaldO.Pia ili kuwazuia madrid ni lazma kumnyima nafasi huyu goal scoring machine(Ronaldo),yote hii itategemea juventus kaba wataweza kushina battle la midfield..kwenye kushambulia juventus wamekuwa wakimtumia Paulo Dybala kama mtu wa kutafsiri mashambulizi yao,dybala anazunguka uwanja mzima,Dybala anafunga na ku assist,huyu ndio key player wa Juventus.
Prediksi-Skor-Juventus-vs-Real-Madrid-4-Juni-2017.jpg

Zidane atakuja na mbinu zake zile zile za kihuni kwenye game kubwa…cha kwanza huwa anajilinda na kushambulia kwa kushtukiza huku akitegemea speed ya Ronaldo benzema na winger mwingine ambaye anaweza kuwa Bale ,Isco,Rodriguez au Asensio...defense ya Madrid itaunganishwa na Casemiro ambaye yuko ki ulinzi zaidi ukilinganisha na Krose na Modric ambapo wao kazi yao ni kufanya Real Madrid inakuwa na mpira na kusambaza mipi haswa kwa Marcelo na carvajaal..

Eneo la kiungo ndilo litakalo amua hiyo game,aamini vita kali itakuwa kwenye kiungo.kwa Juventus watakuwa na kazi ya kuwazuia Kroos na Modric wasiweze kupiga pasi ambazo zitawafikia Marcelo na Carvajaal.

Kwa upande wa ulinzi real Madrid wana tatizo kiasi…goalkeeper K.navas amekuwa na makosa madogo madogo…pia wamekuwa wakiandamwa na majeraha haswa pepe,varane na Marcelo ambayo imepelekeaa Nacho Fernandez kupata nafasi ya kucheza msimu huu Ni wazi kuwa game itakuwa ya nguvu na kasi huku real Madrid wakitawala mchezo na juventus watajilinda na kushambulia kwa kushtukiza…

Ronaldo na Dybala ndio watu ambao nategemea wataamua mechi ingawaje kwenye mechi kama hizi ingawaje mchezaji huwa yeyote anaweza kuamua mechi.. Pia kwenye hii game nadhani ndipo mahali ambapo buffon na ronaldo wanatakiwa kutuonyesha nani kati yao anastahili tuzo ya mchezaji bora wa dunia japo ronaldo ana nafasi nyingine ya kuonesha uwezo wake kwenye kombe la mabara mwezi june nchini Russia

Juve wanakumbukumbu ya mwaka 1998-5-20 walipofungwa na Madrid 1-0

Katika fainali ile ambayo Juve ilipoteza ilikuwa na Zidane(Mchezaji wa Juve katika fainali ile) na kikosi kilikuwa kama ifuatavyo

View attachment 517327

Baada ya kukutana mwaka 1998 watakutana tena Katika fainali ya jumamosi hii ambapo mchezaji wa Juve wakati huko Zidane akiwa upande wa pili wa shilingi

Timu yeyote inaweza kupata ushindi katika fainali hii hivo tungojee tuone uhondo huu kutoka Cardiff,Wales

Makala imeandaliwa na Dkileo na Deadbody

Mimi Deadbody Nipo Juventus na naona fainali hii Juventus 1 VS Madrid 0

FT (1-0)
Fainali ya 1998 iliwaliza sana Zidane na Edgar
 
Sijaona Team ya kuifunga Juventus kwa msimu huu.
Team Juventus, Ushindi nje nje.
 
Back
Top Bottom