Kuelekea ndoa...

kaka muoaji ni wewe alal in all yoyote yatakayotokea uwe tayari ................hawa dada zetu a.k.a hata umwoe sista wivu wanao ......sasa wewe simama katika mstari wako umpendaye ndio chaguo lako wape wao nafasi kidogo ya ushauri lakini wewe ndie final say.....................
 
Kijana anaeamua kuoa ni wewe,ndugu wanafuata baadae,ila uwe jasiri na ukabiliane na changamoto maana hautaweza kuishi bila kushirikiana na ndugu zako,uwe makini kijana!
 
Mawifi wengine bana, usikute wameanza kumchukia sababu tu, waliomba labda kitu fulani wakanyimwa, au zamani ulikuwa unawashirikisha kwenye vitu vyako na sasa huwashirikishi tena na hauwashirikishi si sababu hawapendi dada zake hapana, kapata mtu wa karibu wa ku share nae vitu muhimu kuhusu maisha
Hapo kijana unatakiwa uwe na maamuzi mazito,waite ukae nao kitako uwaulize ni nini kimewachukiza ukiweke sawa na uendelee na mpenzi wako, ndugu wanaweza wakakufanya ushindwe kuishi na mpenzi wa maisha yako, usiwape nafasi waeleweshe kwamba huyo ndio umemchagua awe mkeo. Wazazi siku hizi hawafatilii mambo kama hayo wanawaacha watoto watafute wenyewe wachumba zao
 
Ushauri, ...umeridhika nae muoe
swala la dada sijui kaka au wazazi kutoridhia huwa lipo tu
lakini at the end of the day maamuzi ni yako sababu
huyo muolewaji hataishi na nduguzo bali ni veve mwenyeve(nimeongea kihindi hapo)

Veve daughter inasema kveli sasa?
 
Mkuu oa tu kama ndugu wanaleta KIWINGU kapange zako kwa Mnyamaniiiiiii....jifanye unawasikiliza Dada zako utaletewa..........................................
 
Wadau wote JF,
Heshima mbele,
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuruni nyote kwa michango yenu ya ushauri mzuri kwa hoja yangu hii mbele yenu, NIMEFARIJIKA KWA NJIA MBALIMBALI ZA KIUSHAURI MLIZONIPATIA NAMI NIMERIDHIKA NAZO.
Nawashukuru sana na daima nathamini michango yenu hapa jamvini, shime.
 
Jaribu kufanya uchunguzi,ni kwa nini mwanzo wampende na sasa wamchukie.kama sababu hazina msingi,usikilize moyo wako.
 
We kwa kuwa ushazama penzini unafkir me nikikushaur utanielewa sasa? Cha msing waskilze ndugu zako,huyo mkeo co nduguyo,umeckia muraa?
 
Back
Top Bottom