Hazard ameambia vyombo vya habari kuwa aliamua kuingilia kat i suala hilo na kwamba atajaribu kuishawishi Chelsea kuafikiana na Real kuhusu uhamisho. (Express)
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametishia kuuza nusu ya kikosi chake baada ya kushindwa na Cardiff. (Sun)
Mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale, 29, huenda asirejea Tottenham kwasababu hana haraka ya kuondoka Real Madrid, kwasababu amesalia na miaka mitatu katika mkataba wake wa £600,000-kwa wiki. (Mirror)
Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23, hatauzwa na Manchester United msimu huu kwasababu amemvutia mmoja wa mwenyekiti mwenza Joel Glazer. (ESPN)