Kuelekea msimu mpya Ulaya tupeane tetesi za usajili hapa

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Nimesikia Hazard tayari sasa ni 100% anakwenda R. Madrid kila kitu Tayari.

Barcelona wanataka kumtoa Phillipe Coutinho kwa Chelsea ili wapate fungu la kuwanasa Lacazzete au Dybala.

R. Madrid hawana haja tena kuendelea na kipa wao Navas,pia Rakitic wa Barca kutimkia AC Milan
 
Hiyo habari ya lacazzete ni kama tetesi za flat earth believers
At least ungekuja na tetesi zenye mashiko Mkuu
 
Vipi kuhusu timu ya Wananchi (Yanga) nasikia ipo 2Billions za usajili kwenye account.
 
Nashindwa kuekezea kwa sana maana sijaelewa maana ya neno sajiri. Bora ungekosea kuandika ndani ila kwenye kichwa cha habari. Unaandika Sajiri?
 
Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu uhamisho wa winga wa miaka 23 wa Ujerumani Leroy Sane. (Daily Record)

Barcelona wameamua kumsajili mshambuliaji Antoine Griezmann ambaye ametangaza kuondoka kwake Atletico Madrid msimu huu wa joto.

Hii ni baada ya klabu hiyo ya Uhispania kuondolewa katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa Ulaya na Liverpool(Marca)

Real Madrid wameonesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, huku United ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo kwa pauni milioni 150. (Independent)

Licha ya tetesi kuwa Real Madrid wamekubali makataba wa pauni milioni £86 kumnunua Eden Hazard, 28, Chealsea bado wanashikilia kuwa hatamuachilia kiungo huyo hadi walipwe pauni milioni 100.(Evening Standard)
 
Hazard ameambia vyombo vya habari kuwa aliamua kuingilia kat i suala hilo na kwamba atajaribu kuishawishi Chelsea kuafikiana na Real kuhusu uhamisho. (Express)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametishia kuuza nusu ya kikosi chake baada ya kushindwa na Cardiff. (Sun)

Mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale, 29, huenda asirejea Tottenham kwasababu hana haraka ya kuondoka Real Madrid, kwasababu amesalia na miaka mitatu katika mkataba wake wa £600,000-kwa wiki. (Mirror)

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23, hatauzwa na Manchester United msimu huu kwasababu amemvutia mmoja wa mwenyekiti mwenza Joel Glazer. (ESPN)
 
Everton wanatafakatri uwezekano wa kumtuma mlinzi wa England wa chini ya miaka 21 Jonjoe Kenny, 22, kwa mkopo msimu ujao, huku Seamus Coleman akitarajiwa kuwa beki wa kulia na safu ya nyuma. (Liverpool Echo)

Manchester United huenda wakatumia pauni £12m kumruhusu mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez ajiunge na Inter Milan kwa mkopo msomaji ujao. (Mirror)

Leicester wanajaribu mpango wa kumrudisha kiungo wa kati wa 22 Mbelgiji Youri Tielemans amabe yuko Monaco kwa mkopo, kwasababu Manchester United na Tottenham wameonesha nia ya kutaka kumnua. (Sky Sports)

Barcelona wanataka kumuuza kiungo mkabaji wa kati Philippe Coutinho, 26, msimu huu wa joto lakini hawatamuachilia aondoke kwa kitita cha euro milioni 100 sawa na (£86.8m). (Sport)
 
Manchester United wamerudi nyuma katika mpango wao wa kumnunua Kalidou Koulibably, 27,baada ya kuitisha pauni £90.(Independent)

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City wana mpango wa kuwanunua walau wachezaji watatu wapya msimu huu wa joto, huku wakilenga zaidi mlinzi wa safu ya kati na mashambuliaji. (ESPN)

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Chelsea Mbelgiji Eden Hazard mwenye umri wa miaka 28- atakamilisha mkataba wake wa pauni £86m na Real Madrid baada ya fainali ya ligi ya Europa. (L'Equipe - in French)
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom