Kuelekea mechi ya VPL' Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar, Safari ya Ubingwa Inaendelea

Wana mikakati mizito sana. Safari hii wamepanga kufika nusu fainali ya CAF CL. Ngoja tuone mana wamesajili kwelikweli. Sisi Yanga tutacheza kesho na Zesco tutawasubiria wao wikiendi ijayo tuone watafanyaje kwenye michuano ya kimataifa ha ha ha ha
Hahahahaaa!!!!!! Walijua kufika nusu fainali ni kama kunywa chai. :D:D:D

Na leo si ajabu kidagaa kikaingia mchanga tena mbele ya Ntibwa.
 
Tumewashika pabaya mwaka huu. Yaani siamini kama mnaeza andika kinyoonge namna hii Ses. :cool::cool::cool:
Si tupo wote kwenye ligi ya TPL? Nilikwambia tutawapakata ndani nje msimu huu, si unajua tena mume mumeo tu hata ukiwa na cheo huko kimataifa ukirudi nyumbani lazima upige goti
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kupigwa leo Ijumaa ya September 13, 2019, baada ya kusimama kwa wiki mbili, ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakapopepetana na Wakata Miwa wa Tuliani, Mtibwa Sugar FC, kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni.

Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC, katika safari yake ya kutetea ubingwa wake, amejidhatiti vilivyo kuhakikisha anadondosha kila timu ya VPL, ambayo atakutana nayo ambapo baada JKT, leo hii ni zamu ya Mtibwa Sugar.

Simba SC chini Kocha Patrick Aussems, imejiandaa kuibuka na ushindi kwa kukusanya alama zote tatu pamoja na kuwapa Wanasimba na Wadau wa kandanda burudani ya kiwango bora kabisa ambacho kilichothibitishwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF.

Utaendelea kupata dondoo kuelekea mechi ya leo....Usikose Ukaambiwa..!

Next Level Simba SC Nguvu Moja
View attachment 1206150View attachment 1206151
Nasikia mnacheza na AS Mtibwa ya Somali land
 
Exactly mkuu, maisha haina hana usawa aisee!

Wengine Klabu Bingwa wamevuja jasho lao huku wengine wakienda kwa kubebwa
Sasa Mtaniii si msingevuja tu hilo jasho . :D:D:D Kama mlishajiona mlivuja jasho yawabidi mshukuru tu sasa sababu kama usemavyo maisha hayana usawa na ndio sababu sisi tunazungumzia mechi na Zesco nyie mnazungumzia habari za Mtibwa. Teh teh
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kupigwa leo Ijumaa ya September 13, 2019, baada ya kusimama kwa wiki mbili, ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakapopepetana na Wakata Miwa wa Tuliani, Mtibwa Sugar FC, kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Turiani
 
Back
Top Bottom