Kuna mdau mmoja alielezea vzr ,ngoja niitafute comment yake
huu mchezo haupo kama wengi wajuavyo . Hawa wenzetu wa dar wametuzidi pakubwa mno ktk huu mchezo, kuna kigezo hapo cha omary john 14 hivi hapo umekielewa hicho kigezo ?
- ngoja nikufahamishe ni hivi, wachezaji wengi wanajiona au wanaitwa mabingwa kwasababu ana namna fulani ya kucheza huu mchezo , lkn katika omary john kila mcheza anatakiwa aanze kete zote 7 za vyumba vya mwanzo yaani anatakiwa aanze
Pasati , nugza , meja , kavimba, taa ya treni , mabano na tege . sasa wachezaji wengi wa mikoani utakuta anajua meja lakini mabano hajua au tege hajui , sasa mikoa iliyotajwa kidogo wanaufahamu juu ya hiyo sheria ya omary- john
Kwanin wanaiita omary- john ni kama njia ya kuwaanzi wachezaji wa wili omary na john ambao walipenda kucheza katika utaratibu huo wa kuanza kete zote za mwanzo na kuzipa majina niliyotaja hapo juu.
- Katika mchezo unaoitwa tege . Kuna sheria imesema watacheza tege 4. kwanini wamesema tege na siyo meja , nugza au pasati ?
ni hivi tege ni mchezo unaotaka mchezaji aanze kete ambayo wachezaji wengi wanaamini ni kete dhaifu kama utaanza na kupelekea ufungwe kirahisi na mpinzani wako. Sasa kwasababu wengi wanajua hii itapelekea sare ziwe nyingi na kupelekea mashindano yawe marefu , hivyo kwa kupendekeza wacheze tege basi tunaweza kuokoa muda kwa kuepusha sare zisiwe nyingi.