Kuelekea Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC dhidi ya UD Songo 'Watapigiwa Mpira Mwingi Mno'

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Asalaam Tanzania na nje ya Tanzania..Karibu katika burudani ya soka ya kiwango cha juu kilichothibishwa na Shirikisho la Kabumbu Barani Afrika CAF, kutoka kwa Simba SC, WanaLunyasi, Mnyama Mkali Mwituni

Kuelekea Ligi Mabingwa Afrika, Jumapili Agosti 25, 2019 Mabingwa wa Nchi Simba SC, wanawakaribisha UD Songo, kunako Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya sare ya kutofungana katika mechi awali ilipigwa nchini Msumbiji.

Kocha Patrick Aussems, amesema Simba SC wapo tayari kufanya kila inavyowezekana katika mchezo huo kufanikisha ushindi dhidi ya UD Songo ili kuweza kufuzu hatua inayofuata.

"Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo. Tunatakiwa kuwa makini tunajua tunakutana timu nzuri na mchezo utakuwa mgumu lakini TUNAJIAMINI". Amesema kocha Patrick Aussems.

•••Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana

WanaSimba, Wanachama, Mashabiki Kindakindaki na mdau wa kabumbu, maandalizi yote kuelekea mchezo huo yamekamilika, kwahivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi kuishangilia mwanzo mwisho Simba SC, ambao wataupiga mpira mwingi mno..UD Songo watautafuta mpira kwa Tochi.

Usikose Ukaambiwa..WeAreSimba SC, NguvuMoja This Is Next Level.
FB_IMG_1566674094511.jpeg
IMG_20190824_224224_718.jpeg
 
Tatizo hizo zilizotangulia tuna mashaka na uwezo wao, huoni kuwa mwaka mmoja tu Simba SC amewabeba wengine..NguvuMoja
Ahahahaaaa kuhusu uwezo usihofu Mkuu,siunaona hata Ulaya watu wamechezea vitasa,kufunga na kufungwa ni kawaida.
 
Asalaam Tanzania na nje ya Tanzania..Karibu katika burudani ya soka ya kiwango cha juu kilichothibishwa na Shirikisho la Kabumbu Barani Afrika CAF, kutoka kwa Simba SC, WanaLunyasi, Mnyama Mkali Mwituni

Kuelekea Ligi Mabingwa Afrika, Jumapili Agosti 25, 2019 Mabingwa wa Nchi Simba SC, wanawakaribisha UD Songo, kunako Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya sare ya kutofungana katika mechi awali ilipigwa nchini Msumbiji.

Kocha Patrick Aussems, amesema Simba SC wapo tayari kufanya kila inavyowezekana katika mchezo huo kufanikisha ushindi dhidi ya UD Songo ili kuweza kufuzu hatua inayofuata.

"Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo. Tunatakiwa kuwa makini tunajua tunakutana timu nzuri na mchezo utakuwa mgumu lakini TUNAJIAMINI". Amesema kocha Patrick Aussems.

•••Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana

WanaSimba, Wanachama, Mashabiki Kindakindaki na mdau wa kabumbu, maandalizi yote kuelekea mchezo huo yamekamilika, kwahivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi kuishangilia mwanzo mwisho Simba SC, ambao wataupiga mpira mwingi mno..UD Songo watautafuta mpira kwa Tochi.

Usikose Ukaambiwa..WeAreSimba SC, NguvuMoja This Is Next Level.View attachment 1189396View attachment 1189397
Asante kwa taarifa Haji Manara!!!
 
Back
Top Bottom