Kuelekea kwenye Nchi ya Viwanda (Food for Thought)

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,478
Kwa Heshima na taadhima nawasalimu wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka (calender year) nimepata wasaha wa kutafakari mustakabali wa nchi yangu. Ikiwa mimi ni miongoni wa watanzania wengi wenye mapenzi mema nimeona si vibaya kufikiri kwa sauti pamoja nanyi mambo machache.

Kwanza kabisa, hii hypothesis ya kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda imezaliwa wapi? je ni zao la mawazo binafsi au ni msukumo wa nguvu za soko na za kiuchumi?
Pili, je tafiti za kiuchumi na kisayansi zimefanyika kujua haswa ni viwanda vya ukubwa gani vinavyo hitajika na ambavyo tunaweza kuvimudu na soko la bidhaa zitakazo zalishwa na hivyo viwanda litapatikana wapi? na

Tatu, Je tunao uwezo wa kuvilinda na kuvitunza viwanda hivyo hili viweze kudumu kufanya kazi yake manufaa yetu na vizazi vijavyo?


Msingi wa hoja hizi umejengwa na ukweli kwamba ujenzi wa viwanda au ufunguzi wa biashara mara zote unasukumwa na nguvu ya soko (market forces). Ikiwa kama mahitaji ya bidhaa na uwezo wa ununuzi (demand and purchase power) vipo, basi hali hizo husukuma uzalishaji na ufunguzi wa viwanda. Lakini ikiwa kama ujenzi wa viwanda unasukumwa na utashi wa kisiasa usioongozwa na tafiti za soko na uhimilivu na ustahimilivu wa viwanda usika ni dhairi kwamba nia ya kuifanya Tanzania kua nchi ya viwanda itabakia kwenye mioyo yetu na siyo vitendo vyetu.

Ni vizuri tukajifunza kutokana na yale yaliyotekea baada ya jitihada za hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere (Mwenye enzi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) kufungua viwanda vingi karibu kila kona ya nchi yetu. Viwanda hivyo havikudumu na viliishia kubinafsishwa na mwisho wake mashine zikauzwa na tukaachiwa magala. Hivyo ni vizuri tukawaza pamoja kwa sauti mambo haya.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom