Kuelekea kustaafu Kikwete: I'll always remember...

Kuelekea kustaafu Kikwete: I'll always remember...

Wana Ukumbi,

Pamoja na mambo mengine ya rais Kikwete, lakini ningependa kueleza mambo ambayo sitasahau kuhusiana na rais Kikwete.

Ingawa mambo yapo mengi, lakini makubwa ni kama yafuatayo:

1. UZALENDO, kwa nafasi ambayo JK anayo kwa sasa. Ni yeye tu kuamua watoto wake waende kuishi nje ya Tanzania.

Lakini kamwe hakuwahi kufanya hivyo, watoto wake wote tunapigana nao vikumbo mabarabarani tu na wengine walisomeshwa shule za kawaida kabisa. Its amazing!

Kwenye baraza lake la mawaziri, karibu 90% ya mawaziri watoto wao wapo nje ya nchi yetu. Same applies kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

2. UHURU, katika awamu ya JK sio tu uhuru wa vyombo vya habari uliimarika, lakini hata uhuru wa mwananchi mmoja mmoja.

Katika awamu ya nne ndio utaweza kukuta kuna watu aina ya Dr Slaa. Otherwise, ingekuwa kipindi cha Nyerere basi zamani mtu kama Dr Slaa angepotezwa kimya kimya tu.

3. KATIBA MPYA, kwenye hili naamini Watanzania wenzangu mtaniunga mkono kuwa JK amethubutu.

Katiba mpya lilikuwa ni hitaji la muda mrefu sana, lakini tunamshukuru mhe rais kutuliza kiu yetu kwa kutupatia katiba. Kwenye hili tukio la kiistoria, jina lako litasimama milele.

Yangu mimi ni hayo ya kumkumbuka JK. Wewe je?
Kwa baya 1 alilofanya jana mkuu yoote hayo yamekuwa deleted., Katiba aliyoleta hatimae mwenyewe ndio ameikanyaga kanyaga Tume aliyoichagua ameipotosha sana na kulta rasimu yake mpyaa, hafai JK ni useless ni mtu ambaye tutamkumbuka kwa mabaya maisha yote
 
Mbona Mwinyi na Nyerere hawakufanya?

Nikuulize swali,enzi za nyerere bajeti ilikua sh ngapi?vyanzo vya pesa vya nyerere vilikua vingapi?na sasa bajeti ya kikwete ni sh ngapi na vyanzo vyake vya pesa n vingapi?ulitegemea nyerere ajenge lami nchi nzima kwa maneno?

Ukilinganisha vyanzo vya mapato vya nyerere(pamba+tumbaku)na alichokifanya,kisha kikwete na vyanzo vyake vya mapato(utalii,uuzaji wa twiga,uuaji wa tembo,madini,kodi,uvuvi,kodi kutoka karibu kwa kila raia nk)na alichokifanya,nyerere au mwinyi bado ni bora kuliko kikwete.

Kikwete anaiongoza nchi ikiwa na vyanzo vingi vya mapato vinavyotumika kuliko watangulizi wake lakini amepruvu failiya,..
 
kwangu mimi Rais Kikwete ndo the best president since independent. sihitaji vyombo vya habari kunishawishi kwa hili. Lakini overall ccm wametuangusha sana tokea uhuru.mathalani, Kikwete anaingia madarakani amekuwa tanzania ikizalisha megawatt 750 za umeme, sasa hivi anatoka na anatarajiwa kutuachia megawatt 3000, mifano iko mingi karibia kila nyanja barabara before zilikuwa km 6000 tu lakini anaondoka akituongozea km zingine 11000, yaani mara mbili. huwa nawahsangaaga sana wanaomponda huyu jamaa. eliimu ya msingi, secondary na higher education. plenty.

Huhitaji kumpongeza wala kumkumbuka hiyo ndio kazi aliyoomba,ila mi nitamkumbuka kama deni la taifa limeongezeka yaani hivyo vyote kafanya kwa mkopo
 
Hizo zako ni miongoni mwa sifa za kiboya especially kwa mburula. Mkuu kweli nawewe ni Great Thinker?
Sasa hao wake wa wenyeviti na makatibu wenu pamoja na dada za viongozi wenu waliopewa viti maalumu utasemaje?
Ridhwani anagombea Chalinze kama wengine tu.
Kikwete kampa ubunge Pro. Muhongo kwa utaalamu wake na sio Ridhwani mtoto wake.

u.n.a.k.a.n.y.a.g.wa wewe
 
Huhitaji kumpongeza wala kumkumbuka hiyo ndio kazi aliyoomba,ila mi nitamkumbuka kama deni la taifa limeongezeka yaani hivyo vyote kafanya kwa mkopo
siwezi kujibishana na taahira anayechangika kutoka mawazo ya kuzimu kwenye red highlight ni proof ya hayo
 
siwezi kujibishana na taahira anayechangika kutoka mawazo ya kuzimu kwenye red highlight ni proof ya hayo

Nakusifukwa kutosoma sentensi nzima ukaamua uweke highlight kile kipande kidogo ukasahau kuwa kuwa kile kipande hakina maana bila kusoma sentensi nzima kwa kadiri nilivoandika mimi,pia nakupongeza kwa kuwa u mjuzi na mambo ya kuzimu,inaonesha umewahi ishi huko,ndio.
 
taja mifano ya hiyo mikataba mibovu. halafu pia usisahau kutaja mikata mizuri ya mtangulizi wake. hebu tuone kama akili za misukule ya kibavicha kama zinafanya kazi sometimes. hizi akili za shake before use ni kazi sana

Mimi wala sitaki kumkumbuka ila ningemkumbuka vizuri kama katiba ya sasa ikiwa na kipengele cha kumshitaki rais kwani nadhani atakuwa Rais wa kwanza kustaafu na kwenda jela kwa miaka yake iliyobaki.

Mikataba yote mibovu yeye na maswahiba wake waliyoingia inayotesa wananchi ipo siku Mwenyezi Mungu ataona vilio na machozi ya watanzania.
 
ni kweli kabisa, hata kule kalenga waislam wameitosa chadema. haa haaa!

Safi sana kwa propaganda ya udini juu ya CHADEMA, propaganda hii inaendeleza utamaduni wa kuwatumia waislam kwa kuvuna kura zao, ni dharau kubwa sana kuwatumia waislam kwa kuvuna kuwatumia kama shamba la bibi, mnawaambia chama fulani cha Kikristu ili muendelee kuvuna kura, hahaha sijui wataacha kutumika lini
 
wewe utakuwa taahira kama sio punguwani. sasa unataka waweke lami mpaka mashambani, vyumbani, baharini kwenye maziwa/mito na maporini ili wanyama na samaki wapite? sidhani kama unaelewa ila kwa kukusaidia tu tanzania inamtandao wa barabara km 84,000. kikwete amekuta zilizojengwa ni 6000 tu na sasa anamalizia jumla ya km 11,000 yaani karibia mara mbili ya watangulizi wake wote kwa pamoja.

Nchi yenye kilometa 945,087 za mraba alafu lami ni km 11000 tu ,alafu unasifia what nonsense is this, ebu kokotoa hapo ujue ni maeneo mangapi hayana Lami na siyo kusifia eti. 945087-11000 means 934087 hamna Lami alafu mtu unaanzisha thread kusifia ujinga. Ungeanzisha Uzi kumsifia kwa kuwa rais alietembelea nchi nyingne duniani hadi kupokelewa na Naibu waziri dah what shameful is that.
 
Safi sana kwa propaganda ya udini juu ya CHADEMA, propaganda hii inaendeleza utamaduni wa kuwatumia waislam kwa kuvuna kura zao, ni dharau kubwa sana kuwatumia waislam kwa kuvuna kuwatumia kama shamba la bibi, mnawaambia chama fulani cha Kikristu ili muendelee kuvuna kura, hahaha sijui wataacha kutumika lini

Vp na kuhusu walaka wa kanisa?
 
Kwa baya 1 alilofanya jana mkuu yoote hayo yamekuwa deleted., Katiba aliyoleta hatimae mwenyewe ndio ameikanyaga kanyaga Tume aliyoichagua ameipotosha sana na kulta rasimu yake mpyaa, hafai JK ni useless ni mtu ambaye tutamkumbuka kwa mabaya maisha yote

sasa mkuu si afadhali yeye amethubutu kuanzisha huu mchakato,,, kushindwa kwa huu mchakato ni yaleyale tunayoyaita african common problem, ubinafsi, unafiki, ujuaji nk. kama wale watu karibu 600 wanashindwa kujua lipi linamanufaa kwa taifa, yeye afanyeje sasa....

NI JUKUMU LA WALE WATU 600 Kuwa wazalendo na kututengenezea katiba KATIBA YENYE TIJA KWA WANANCHI....
 
Kuuleta ama kutouleta huu mchakato wa Katiba kwa sasa it is good for nothing Jk he is a snake in the grass wajumbe 600 unaozungumzia kabla ya yeye walikuwa na mitazamo tofauti kulingana na maoni ya watanzania, sasa wamelazimika kufuata kauli na maoni ya Mkuu wa Nchi, tayari Jk amejenga hofu kwa wajumbe wa bunge maalum,, sasa wajumbe hata hawo wa ccm hawataangalia tena rasimu wataangalia Rais amependekeza nn, ni hatari jk mbaya sn ameuwa Taifa dakika za mwisho., tutamkumbuka kwa ubaya sanaa
 
Back
Top Bottom