Kuelekea April 01, uchaguzi Arumeru...

Kuelekea April 01, uchaguzi Arumeru...

Ushindi wa timu hautegemei idadi ya mashabiki. Habari kutoka uwanja wa Manumbu zinasema kundi kubwa la wachezaji hasa vijana hawana jezi, wameisha ziuza. Mnunzi anatangaza dau kubwa, taarifa zinasema jezi moja inanunuliwa hadi 50,000/= kwa mchezaji anayeonekana kupinga kuuza jezi yake. Hilo, mnalifanyia kazi ? Mkishinda hilo, basi mmeweza. Fanya sampling katika mikutano, uliza baadhi ya wachezaji wakuonyeshe jezi zao, utaomba dunia ipasuke uingie.
 
Nafikiri siku ya tarehe 1/4/2012 kuanzia saa 12 jion tutapata ukweli chama gani kiliuza sera vizuri kwa wananchi wa arumeru mashariki.
 
wajameni tunataka tathimini za ukweli kama tunazika ccm au la
 
nimepata tathmini kutoka kwa mdau anayeshiriki mchakato wa kampeni za ccm huko arumeru east na ameniambia kuwa hali ya chama hiko ni mbaya sana.

Maeneo ambayo ccm imeendelea kuungwa mkono ni pamoja na kata zifuatazo;
NKUARISAMBU-huku anatoka diwani wa ccm ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya meru.

MBUGUNI-diwani wa mbuguni ni maarufu sana bw thomas laizer au 'askofu' ingawa kuna baadhi ya watu wana wasiwasi na kata hii kwani askofu alipata kashfa ya rushwa hivi karibuni.

MARORONI na KINGO'RI-madiwani wa kata hizi ni maarufu na wanaheshimika kwa kazi yao.

Jumla ya kata huko arumeru ni 17.

Tathmini yako imekaa bjb hali ya kutungwa tungwa na kushindwa kuwa makini ktk utunzi wako na umeiacha inaelea elea
 
Cdm wanaumiza kichwa jins yakuwashawishi wananchi ili wawape kura na ccm wanapanga njama za kuiba kura kweli siasa za TZ zina mambo!!?
 
Hiyo tathmini haina mashiko,Mwenyekiti wa halmashauri ya meru,ni diwani wa kata ya وLeguruki sio Nkoarisambu,King'ori diwani wa huko hana lolote,ni Baba yangu Mkubwa amekuwa diwani kwa miaka 30,tena kwa kuhujumu hujumu tu,ndio kata natokea,tumefanya kazi kubwa sana,na uhakika wa kuchukua kura zote kwenye hii kata ni mkubwa,Mbuguni,askofu ana kesi mahakamani dhidi ya wapiga kura wake,yaani wananchi wamemshitaki mahakamani diwani wao kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka,na ubadhirifu.Kimsingi kila kata ina hoja,hivyo CHADEMA tunawashinda mapemaaaaa
Well said!...pamoja sana mkuu!
 
Mungu awe nanyi kuonyesha njia ya mabadiliko !
 
Back
Top Bottom