Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,596
- Thread starter
- #21
Mwaka 2015 ndio huu, sasa Chadema imepata dereva mzoefu anayeijua njia, na CCM iko vile vile na ule mkweche wake!, there is no way CCM inaweza kushinda!, unless ni by means of hooks and crooks!.Wanabodi,
hivyo mshindi wa jumla wa urais 2015, ataendela kuwa ni CCM!, "Unless Otherwise!". Huu ndio ukweli mchungu!.
Chadema inayo nafasi ya kushinda kama itakubali "to do things right", kwa sasa kupitia M4C, Chadema, inafanya kazi nzuri ya kuwaamsha Watanzania kujua haki zao!, yaani "is doing the right thing!". Lakini ili chama kipya kiweze kuking'oa "chama kubwa", "chama kongwe" madarakani na kuingia Ikulu, "doing the right thing" peke yake hakutoshi!, it got to do "things right", kitu ambacho sikioni Chadema kufanya mpaka sasa,hivyo kila mara nimekuwa nikiwashutumu kuwa "Chadema Haijajipanga!" na labda kwa vile mimi sio mmoja wao, inawezekana kabisa wakawa wanajipanga, kimya kimya, ndani kwa ndani, ili siku ya siku wakiibuka, ni surprise attack au "ambush" ya "funika bovu!" moja kwa moja hadi Magogoni!, hiyo ndio ile "unless otherwise!", lakini kwa hapa tulipo kuelekea 2015, Watanzania (kama mandondocha vile), tutaendelea kuichagua CCM kwa mazoea!.
Siasa ni kama barabara ndefu, mbovu na ya kona kona, milima, mabonde, mashimo na makorongo!, vyama ni kama magari, wanachama ndio abiria, na viongozi wa vyama ndio madereva!. Kuelekea 2015 ndio safari yenyewe. Kwa huku bara, mchuano ni kati ya CCM, (gari kongwe, injini kongwe chovu, lakini dereva mzoefu, aliyeisha izoea hiyo barabara, miaka nenda, miaka rudi, hivyo anajua aendesheje, wapi apunguze mwendo na wapi aende kasi, wapi kuna korongo wapi kuna bonde, wapi kuna konakali na wapi kuna mlima, etc,etc!) na Chadema (gari mpya na injini bomba ina kasi kupita ule mkweche ila ina dereva mpya ambaye hajui sana hiyo njia!, kazi ya dereva mpya ni kutimua mbio tuu na kututimulia vumbi!, na kuendesha kwa kasi ili awahi kufika!, kutokana na kutojua vizuri njia, japo anakwenda kasi zaidi, kwa kuipita gari kongwe kwa mbali ambayo ni spana mkononi, mara kibao hujikuta anapotea njia, hivyo kulazimika kurudi nyuma na kuendelea na safari!.
Kwenye hii scenario, huyu dereva mpya anayo nafasi ya kushinda, sio kwa kitimua mi mbio tuu, bali endapo atakubali kuelekezwa kuhusu hiyo njia na wazoefu, au kuwasikiliza baadhi ya abiria wake wazoefu ambao wameishaipita njio hiyo mara nyingi ndani ya ule mkweche, au kutusikiliza sisi watazamaji wa mchuono huo ambao sio abiria wa gari yoyote, ila tuko humo njiani kwa muda mrefu, tunapoona dereva mpya anakosea, huwa tunampungia ishara kuwa huko siko!, au kumpa ishara ya hatari ya mbele, lakini dereva huyu, kutokana na kuhamanika na ushindi, na kelele za chagizo za wale abiria wake ambao wanashangilia ushindi njia nzima kwa morali ya hali ya juu, dereva hasikii wala ishara za hatari hazioni, yeye ni mwendo mdundu kuelekea mwisho wa safari kwenye ushindi tuu!.
Safari ya kuelekea 2015 ndio hii inaendelea, sasa hivi tuko half way!, bado hakuna dalili za dereva mpya kujifunza!, nasikia kutafanyika zoezi la kubadilishana madereva baadae mwaka huu, hebu na tusubirie timu mpya tuone kama kuna mabadiliko!, na hata kama ikirudi timu ile ile, basi ni lazima ibadilike! kama itaendekeza uendeshaji ule ule, basi ni hakika bila mashaka yoyote, mshindi ataendelea kuwa yule yule, dereva bingwa mwenye gari bovu!, yaani yule yule mwenye ule ule mkweche!.
Kwa maoni yako, katika hii safari ya kuelekea 2015, jee dereva mpya, mwenye gari mpya, mashine bomba ambaye hajaizoea njia, anaweza kumshinda dereva mkongwe, mzoefu wa safari, mwenye gari bovu, na mkweche?!.
Wito wangu kwa wapenda mabadiliko wote!, fuatilieni kwa makini hii trend iliyopoi sasa!, 2015 msije kushangaa!.
Wasalaam.
Pasco.
Kwa ajili ya reference, inaweza pia kupitia hizi threads.
Pasco