Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
JANUARI 29, 2016 majangili wakitumia silaha nzito ya kivita aina ya AK47 walimpiga risasi na kumuua rubani Kapteni Roger Gower (37), pamoja na kuiangusha helikopta ambayo ilikuwa ikifanya doria katika pori la akiba la Maswa wilayani Meatu katika Mkoa wa Simiyu.
Kapteni Gower, raia wa Uingereza, alikuwa akiongoza chopa hiyo iliyokodiwa na kampuni ya Mwiba Holdings Ltd akiwa na msaidizi Nicky Bester, raia wa Afrika Kusini katika harakati za kuwasaka majangili walioua tembo watatu kwenye pori hilo.
Watu tisa walikamatwa na kushtakiwa wakihusishwa na tukio hilo. Washtakiwa hao ni Iddy Mashaka (49), Shija Mjika (38), Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42), Moses Mandagu (48), Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40), Mapolu Njige (50) na Mange Barumu (47).
Tayari Mahakama ya Wilaya ya Bariadi imekwishawahukumu washtakiwa wanne kati ya tisa kifungo cha jumla ya miaka 70 jela kutokana na tukio hilo huku washtakiwa wengine kesi zao zikiendelea. Hukumu hiyo ilitolewa Februari 11, 2016 na Hakimu Mary Mrio wa mahakama hiyo.
SOMA ZAIDI...