Kudumisha long distance relationship -part 1

Kudumisha long distance relationship -part 1

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,341
Ni sehemu ndogo sana ya wapenzi wanaoishi mbalimbali ambao hudumu katika uhusiano wao kwa muda mrefu. Hiki kinaonekana kuwa ni kitendawili kigumu sana kwa wapenzi wengi kuvumiliana kwenye uhusiano bila kusalitiana.

Ninapozungumzia umbali namaanisha wilaya na wilaya, wilaya na mkoa au mkoa na mkoa au nchi na nchi au bara na bara.

Ninaamini miongoni mwetu ama tumeshuhudia au kusikia au kuona au kuadithiwa kuwa kuna mwanaume au mwanamke ambaye alikuwa na mpenzi, mara mpenzi wake akapata nafasi ya kwenda kusoma mkoa mwingine au nchi nyingine lakini mwisho wa siku ukasikia wapenzi wale wamemwagana baada ya mmoja kupata mpenzi mwingine huko aliko.

Inawezekana mpenzi wako alihamishwa kikazi nje ya wilaya uliyopo lakini mwisho wa siku ukabaini kuwa mwenzio amepata mtu mwingine na mapenzi kwako yameanza kupungua au yamepungua kama siyo kwisha kabisa.
Najua wengi huwa mnajiuliza ni nini huwa kinachangia? Zifuatazo ni baadhi ya sababu;

Kutokuwa na uaminifu miongoni mwenu, kama wapenzi mtakuwa ni waaminifu katika uhusiano wenu basi kila unapoingiwa na pepo wa usaliti unakumbuka uzuri wa mpenzi wako basi unaacha na kujizuia kumshinda pepo huyo.

Kutokuwa mzalendo kwa mpenzi wako. Jaribu kumpenda kwa kuwa ndiye uliyemchagua kuwa naye, kila siku Tanzania inasema watumishi wake wawe wazalendo, siyo wao tu hata mapenzi yanahitaji uzalendo.

Uzalendo wa kupenda kitu chako, kumpenda mpenzi wako, mkeo, mumeo au mchumba wako. Lazima ujivunie, ujisifie kuwa naye kisha mthamini.

Kutokuwa na subira au uvumilivu. Hili nalo huchangia mapenzi ya mbali kuvunjika. Kama ilivyo subira ya kila mtu kuamini kuwa ipo siku ataondoka kwenye shida na ugumu wa maisha alio nao, basi amini na kuwa na subira au uvumilivu kwa mpenzi wako ili mfikie ndoto zenu.

Jiepushe sana na mazingira ambayo yanaonekana kabisa yanaweza kukusababisha ukaingia kwenye uhusiano usio rasmi tena, pengine kwa mtu ambaye huna ndoto naye.Tatizo la kujiingiza kwenye uhusiano kwa sababu za kimazingira linaweza kukufanya ukajikuta umezama kwenye huba na mtu ambaye hana mapenzi na wewe na mwisho wa siku ukajikuta unaumia sana.

Kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nayo huchangia sana kuvunjika kwa mapenzi ya mbali au kupoteza ladha, lakini kama mtu anakupenda, anakupenda tu, anaweza kukupigia simu na kukutumia SMS kibao lakini akawa bado ni tatizo.

Kama utaishi kwa kutamani vitu usivyokuwa na uwezo navyo ni dhahiri utajikuta unamsaliti mpenzi wako kwa kuwa tu uko mbali na unaona hawezi kukubana wala kukufuatilia. Ingawa ningeshauri ufanye kitu kwa kujiongoza na siyo kwa kuongozwa na tamaa au kwa kuwa mpenzi wako hayuko karibu nawe.

Acha maisha ya kufuata mkumbo kama mwenzako amefanya kitu flani basi eti na wewe unataka ukifanye au ukipate ili uonekane wa kisasa au mjanja.
Kumbuka kuwa mwisho wa siku mtamaliza chuo na mengineyo, kila mtu atasambaa, kama uliharibu kwa mpenzi wako, mwenzio hatokuwepo.
 
Kama kweny long distance trade kulikuwa na pesa na bado ikafa hivi hizi long distance relationship zitadumu kweli??
 
fimbo ya mbali haiui nyoka, unadumisha mawasiliano kupiga simu/texts halafu anazijibu akiwa kifuani kwa jamaa, long distance relationship ni wizi kama BIKO tu
 
fimbo ya mbali haiui nyoka, unadumisha mawasiliano kupiga simu/texts halafu anazijibu akiwa kifuani kwa jamaa, long distance relationship ni wizi kama BIKO tu
Mawazo ya mwanadamu hayawez kua sawa na mipango ya Mungu
 
LDR sio rahisi kama tunavyodhani ila ni kweri hizo sababu zoote zipo sahihi na pia mapenzi ya kweli yanaweza kuwepo na kudumu,

mimi nipo mbali na mpenzi wangu njia kuu ni mawasiliano hasa video call na kipindi cha likizo ndefu either aje au niende....

ni kuwa serious tu! kuna point hapo umezisema..yani ukiona unashawishka kumsaliti mpenzi wango jiulize

"is He/She worth loosing the one you have..!!?"

tatizo vijana tunaendekeza sana tamaa, tuwe na misimamo.

Asante chief kwa kunikumbusha.
 
apo kwenye video calls.. dah! a friend alikua anawasiliana na mwenzie kwa video calls ila anaweka sura tu kumbe tayari ana mimba.. calls every day paka anajifungua.. mahusiano ya mbali kweli yanahitaji moyo!
 
hatari sana, Mungu atusaidie kwakweli
 
Back
Top Bottom