Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
SIKU moja baada ya serikali kutangaza kuwa, itaanza kuchapisha nyaraka za kupigia kura nchini, kwenye chaguzi zijazo, wabunge na madiwani wa CUF wamedai kuwa, hiyo ni mbinu nyingine ya kukipa chama tawala ushindi wa tsunami.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Lipumba, aliiambia Mwananchi jana kuwa, serikali imebuni mbinu hiyo baada ya kugundua kuwa, upepo wa kisiasa katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Oktoba 2010, utakuwa mbaya kwa CCM na kuwepo uwezekano wa kushindwa.
�Utaratibu huu wa kuchapisha karatasi za kura nchini, unaonyesha dhahiri kuwa unalenga kuisadia CCM na kwa mbinu hii itapata ushindi wa tsunami, tofauti na ule wa kishindo wa mwaka 2005,� alisema Prof Lipumba.
Prof Lipumba alifafanua kuwa, kitendo cha serikali kutoshirikisha vyama vya upinzani katika mazungumzo yoyote ya uanzishwaji wa utaratibu huo, kinaonyesha kuwa ina lengo la kuipendelea CCM.
�Na kwa vyovyote vile CCM itakuwa iliujua mapema mpango huu wa kuchapisha karatasi za uchaguzi nchini na kwa hiyo imeshajipanga,� alisema Prof Lipumba.
Pia Profesa Lipumba alisema ana shaka na usalama utakaokuwepo wa kuzitunza karatasi hizo.
�Sijui utunzaji wa karatasi hizi utakuwaje, maana serikali inayotawala ni ya CCM na sisi kama wapinzani hatujashirikishwa katika lolote,� alisema Prof Lipumba.
Serikali imesema itaanza kuchapa karatasi hizo ndani ya nchi, baada ya kupatikana kwa mitambo mipya na ya kisasa yenye uwezo wa kuweka alama za siri, namba na rangi katika karatasi za kura kwa usalama mkubwa na uwezo wa kuhakiki alama za siri zitakazowekwa.
Kazi hiyo itatekelezwa na Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali, ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Tume ya Uchaguzi ya(Nec).
Ununuzi wa mitambo hiyo, ni mpango wa serikali wa kutaka kuimarisha idara hiyo tangu mwaka jana na serikali ilitoa zaidi ya Sh1.7 bilioni kwa ajili ya idara hiyo na mwaka huu imetenga zaidi ya Sh1 bilioni ili kutekeleza mpango huo, ambao unaondoa gharama kubwa za kuchapisha karatasi hizo nje ya nchi.