Kuchangia kwa hiari ujenzi barabara ya Msongola jimbo la Ukonga

Nendubotho Sunguya

Senior Member
Oct 9, 2019
126
112
Habari wanajukwaa.

Kwa dhati ya moyo wangu ninalileta jambo hili mikononi mwenu nikiamini linawezekana.

Kama unatokea Mbagala kuna kipande kutokea Mbande mpaka Msongola (kilimo) ambacho sio kwamba tu hakina lami bali ni mashimo na makorongo yasiyohimilika kabisa.

Kero hiyo ya barabara imegeuza taswira ya huku kabisa. Magari hayafiki, bidhaa ni ghali mno na kero nyingi zitokanazo na ubovu wa barabara.

Tulishalia na Mbunge wetu na viongozi mbalimbali lakini danadana zimekuwa nyingi sana. Sasa barabara hii kwa hichi kipande korofi ni takribani kilometa 5 kwa makadirio.

Nimeongea na baadhi ya watu, viongozi wa ngazi za chini (ambao wanafikika), tumeona tuchange wananchi wa eneo hili walau pesa yoyote ile watu waliyonayo tutengeneze mfuko kwa ajili ya ujenzi wa baraabara hii.

Tukaja pia na wazo la kushirikisha viongozi wa juu kama watapatikana tuone wanatusaidia vipi. Pia kuna mmoja wetu ametoa wazo la kufungua Go fund me page kwa ajili ya ujenzi wa hii barabara.

Nafahamu inahitajika pesa nyingi sana, lakini hata tukiraise kiasi kidogo cha fund itakuwa ni meseji kwa watu na viongozi huko juu akiwemo Rais wetu.

Hili jimbo limesahaulika na hakuna dalili yoyote ya matumaini.

Nawakaribisha kwa mawazo yenu nini cha kufanya maana tunahitaji hili jambo liwe katika hali nzuri tukifanikiwa pesa isipigwe.Maana tuliokaa na kulizungumza hili hamna kiongozi zaidi ya mmoja wa kata.

Nitaattach picha zaidi ya eneo.Kwa mawazo namna ya kufanya hili lifanikiwe nakaribisha maoni hapa au pm au kwa njia ya simu.+255766523890

Asante.

20191021_123146.jpg
 
Hongera mkuu kwa uhamasishaji.
Ila kwa usalama wa fedha na jambo hili kuaminika lingefanywa na Viongozi kama diwani au Mbunge.
Mkuu lakini kuna mfuko wa barabara wakumbusheni viongozi wenu waweke kwenye mpango kufanya ufuatiliaji.
Mkuu pia kuna TARURA waoneni wanaweza kusaidia.

***ila mbunge huko si aliunga mkono juhudi hadi kumfanya kuhama chama, mlipaswa muwe mna maendeleo aliounga mkono..
 
Mkuu umeongea hivi ni kama umeniamshia machungu ya kutaabika barabara yetu ya kivule huku asee ni tabu tupu. Viongozi husika hususan mbunge wa jimbo mh Waitara ndio hana kabisa habari na hii barabara, sasa sijui ndio uwakilishi gani huo wa wananchi

Kama ulivosema, jimbo hili ni kama limesahaulika kweli kabisa au wanachukulia km ni sehemu ya kutimizia wanachokitaka, wapige pesa kisha wasepe ndio tz yetu ilivo sasa

Me nashauri badala kuhangaika kuchangishana pesa hapo dawa ni kufanya mobilisation na kupaza sauti zaidi ili tatizo hili lionekane kila sehemu na kwenye kila social network. Nadhani itasaidia
 
Mi najua watanzania kwa kuchangia harusi ni wepesi sana lakini maendeleo ni ngumu sina hakika kwa wafanyabiashara wanaotengeneza faida kwa huo ubovu kama watachangia ,na ni vyema huyo mbunge akalibeba hilo jukumu zaidi na diwani wake!
 
Nitaattach picha zaidi ya eneo.Kwa mawazo namna ya kufanya hili lifanikiwe nakaribisha maoni hapa au pm au kwa njia ya simu.

Asante.

View attachment 1241452
Mtumie picha mzee baba kua wananchi wa huko wote ni ccm utaona kesho barabara inatengenezwa,mana hiyo barabara utafikiria uko msitu wa congo
 
Hongera mkuu kwa uhamasishaji.
Ila kwa usalama wa fedha na jambo hili kuaminika lingefanywa na Viongozi kama diwani au Mbunge.
Mkuu lakini kuna mfuko wa barabara wakumbusheni viongozi wenu waweke kwenye mpango kufanya ufuatiliaji.
Mkuu pia kuna TARURA waoneni wanaweza kusaidia.

***ila mbunge huko si aliunga mkono juhudi hadi kumfanya kuhama chama, mlipaswa muwe mna maendeleo aliounga mkono..
alishakuja kwenye mkutano tukamuuliza hii barabara vipi akasema atajaribu kuomba kama walau atapata kifusi.
mbunhe huyo Waitara.
Naamini CCM itatupa watu wengine makini uvhaguzi ujao.
mbunge wetu ndo maka hivyo
madiwani wapo kimyaa kabisa
na Mkuu wa wilaya (wilaya ya ilala) ndo alionekana kipindi cha kampeni wakati waitara kahamia CCM.
kwa kifupi hatuna wa kumlilia yaani huku hali ni mbayaa kweli kweli
 
Halafu kesho utajifanya unagombea udiwani kwa tiketi ya CCM wakati hela ya ujenzi umetuchangisha Asubutuuuuuu
Mkuu hayo ni majaliwa ya mwenyezi Mungu lakini lengo sio hilo kabisa
hali huku ni mbaya sana Mkuu.
tunaomba michanho yenu ya hali na mali
 
Mkuu umeongea hivi ni kama umeniamshia machungu ya kutaabika barabara yetu ya kivule huku asee ni tabu tupu. Viongozi husika hususan mbunge wa jimbo mh Waitara ndio hana kabisa habari na hii barabara, sasa sijui ndio uwakilishi gani huo wa wananchi

Kama ulivosema, jimbo hili ni kama limesahaulika kweli kabisa au wanachukulia km ni sehemu ya kutimizia wanachokitaka, wapige pesa kisha wasepe ndio tz yetu ilivo sasa

Me nashauri badala kuhangaika kuchangishana pesa hapo dawa ni kufanya mobilisation na kupaza sauti zaidi ili tatizo hili lionekane kila sehemu na kwenye kila social network. Nadhani itasaidia
Nashukuru mkuu kwa mchango wako.
hili ni wazo zuri sana.
kama iyaweza nitumie picha za barabara eneo ulipo kwenye wasap au attach katika uzi huu.na taja eneo ulipo.
Jimbo limesahaulika hili ni kila mahali mkuu barabara ni mbovu sana.
huko kitunda nako hali ni mbaya sana.
wamezoea Wananchi kunyamaza kila mara na kuwaacha aaendelee kuwa wabunge kama picha tu
namba ya wasap
 
Mi najua watanzania kwa kuchangia harusi ni wepesi sana lakini maendeleo ni ngumu sina hakika kwa wafanyabiashara wanaotengeneza faida kwa huo ubovu kama watachangia ,na ni vyema huyo mbunge akalibeba hilo jukumu zaidi na diwani wake!
Mbunge ni Waitara mkuu
watanzania tuamke tuchangie meendeleo zaidi kuliko starehe.
 
Kazi ya kujenga Barabara ni ya Serikali sababu ndiyo inakusanya kodi.
Haitengenezwi sasa tunazidi kuteseka wananchi.lakini pia kuna hospital zimejengwa na wananchi kuna Shule n.k
lakini japo serikali ina jukumu la kutengeneza .
 
Yani mi nitoe hela niijengee tarura barabara, zile faini wanazokusanya kwene malori wazielekeze huko, nasikia waitara ukimuuliza habari za maendeleo anakununulia bia
 
Nashukuru mkuu kwa mchango wako.
hili ni wazo zuri sana.
kama iyaweza nitumie picha za barabara eneo ulipo kwenye wasap au attach katika uzi huu.na taja eneo ulipo.
Jimbo limesahaulika hili ni kila mahali mkuu barabara ni mbovu sana.
huko kitunda nako hali ni mbaya sana.
wamezoea Wananchi kunyamaza kila mara na kuwaacha aaendelee kuwa wabunge kama picha tu
namba ya wasap +255766523890
Ni kweli mkuu, ntakuchek wasap yako kwa ushirikiano zaidi kwenye hili
 
Habari wanajukwaa.

Kwa dhati ya moyo wangu ninalileta jambo hili mikononi mwenu nikiamini linawezekana.

Kama unatokea Mbagala kuna kipande kutokea Mbande mpaka Msongola (kilimo) ambacho sio kwamba tu hakina lami bali ni mashimo na makorongo yasiyohimilika kabisa.

Kero hiyo ya barabara imegeuza taswira ya huku kabisa. Magari hayafiki, bidhaa ni ghali mno na kero nyingi zitokanazo na ubovu wa barabara.

Tulishalia na Mbunge wetu na viongozi mbalimbali lakini danadana zimekuwa nyingi sana. Sasa barabara hii kwa hichi kipande korofi ni takribani kilometa 5 kwa makadirio.

Nimeongea na baadhi ya watu, viongozi wa ngazi za chini (ambao wanafikika), tumeona tuchange wananchi wa eneo hili walau pesa yoyote ile watu waliyonayo tutengeneze mfuko kwa ajili ya ujenzi wa baraabara hii.

Tukaja pia na wazo la kushirikisha viongozi wa juu kama watapatikana tuone wanatusaidia vipi. Pia kuna mmoja wetu ametoa wazo la kufungua Go fund me page kwa ajili ya ujenzi wa hii barabara.

Nafahamu inahitajika pesa nyingi sana, lakini hata tukiraise kiasi kidogo cha fund itakuwa ni meseji kwa watu na viongozi huko juu akiwemo Rais wetu.

Hili jimbo limesahaulika na hakuna dalili yoyote ya matumaini.

Nawakaribisha kwa mawazo yenu nini cha kufanya maana tunahitaji hili jambo liwe katika hali nzuri tukifanikiwa pesa isipigwe.Maana tuliokaa na kulizungumza hili hamna kiongozi zaidi ya mmoja wa kata.

Nitaattach picha zaidi ya eneo.Kwa mawazo namna ya kufanya hili lifanikiwe nakaribisha maoni hapa au pm au kwa njia ya simu.+255766523890

Asante.

View attachment 1241452
safi good idea
 
Back
Top Bottom