Kuboresha mahusiano

Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
24,685
28,769
Hii nimeikuta mahali nikaona si mbaya nikishea humu mana kila mmoja wetu anahitaji mahusiano yake yanoge

DONDOO KUMI KWA WANAUME ILI KUTENGENEZA MAHUSIANO YENYE AFYA.

1. Usijisahau katika mahusiano ukawa comfortable kiasi kwamba zile mbwembwe zote za kipindi unamtongoza ukazipotezea. Mwanaume smart haachi kumfanya mwanamke wake ampende zaidi. Mwanaume anaemfanya mwanamke wake ampende zaidi mahusiano yao hudumu mpaka uchweo.

2. Usisahau kufanya tabasamu kuwa kipaumbele cha mwanamke wako. Ole wao wanaume wanaowanyima tabasamu wapenzi wao wakaacha wanaume wengine ndio wawape tabasamu wanawake zao. Nawaambien mpo kwenye matatizo makubwa.

3. Yatunze maneno yako kwa uaminifu mkubwa. Uaminifu ni msingi imara wa mahusiano yenye afya. Mwanaume wa kweli hakimbii majukumu.

4. Usiwe mkoloni katika mahusiano. Kuna haki ya kusikiliza na kusikilizwa (natural justice). Kuwa mwanaume, admit kama umekosea. Kuwa na ujasiri wa kurekebisha pale ulipokosea

5. Usimfanye mwanamke wako aone kama anashindana na muda wako, mfanye ajisikie na yeye anathamani katika muda wako. Sio sababu ya kuwa na muda au laa bali ni jitihada ya wewe kutengeneza muda wa pamoja.

6. Usiwe mvivu. Kuna mtu mwingine pembeni ambaye anatamani kuwa na huyo mwanamke. Linda tunu yako kwa upendo, furaha na amani nae. Usiwe mvivu kumfurahisha, kumlinda, kumridhisha na kumsifia. Pombe na nyama choma zisije zikakuponza.

7. Usihukumu. Kila mmoja anafanya makosa na anajifunza kwayo. Usihukumu makosa yake wala past yake. Na kitu cha muhimu usimhukumu kwa vile unafikiri tofauti na yeye. Binadamu tunatofautiana sana. Enjoy kuwa nae kwa jinsi alivyo. Usilazimishe awe kama wewe.

8. Usi assume kwamba anajua kama unamjali, mwonyeshe kweli unajali. Mpe support katika shughuli zake i.e masomo, biashara, kilimo, etc. Mtumie sms, msikilize, msifie, muonyeshe mapenzi kwa maneno na vitendo na uwe mbunifu.

9. Usiwe mwanaume jina, acha tabia ya kuzila na kususa ,onyesha kuwa wewe ni mtu wa majukumu na ni kichwa katika mahusiano, jenga mahusiano kwa busara zaidi na sio kwa ki imla (dictatorship). Maumuzi yako ya kijinga kijinga yatakutokea puani.

10. Usikate tamaa kirahisi, najua maisha ni magumu ila mwanaume wa kweli anapotaka kitu, atafanya kila awezalo kukipata, unasubiri nini? fanya hivyo sasa.

BUSARA KWA WANAWAKE. YAFUATE HAYA MAHUSIANO YAKO YADUMU.

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubutu wako.

2. Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani kuwa nae.

3. Tabia yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.

4. Kuwa mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio kuwa mtu wa kulipiza visasi.

5. Kuwa kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa mumeo. Hiyo ni busara.

6. Usiweke mashindano na mumeo, mpe hongea na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika maisha.

7. Kuwa na ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't help u!

8. Kuwa mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.

9. Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.

10. Hakuna kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.

11. Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.

12. Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu atakubariki.

13. La mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakin yule mwenye maarifa na ufahamu yeya afaa kwa maisha yote!
 
"MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME"
Neno hili Wanaume wengi huwa tunalitafsiri vibaya pale Muhusika anapoanza kuifanya kazi yake Kikamilifu.
Ukiona Mkeo anakuambia "Sipendi na staki uendelee kuchat na wadada flani" au Sina "Amani na Rafiki yako flani naomba uachane nae tabia zake sio nzuri"
Wanaume wengi wa kileo maneno haya huona kwao kama bugudha na hasa huisi wenzi wao wanataka kuwakalia au kuControl maisha yao.
Ngoja nikwambie kitu muhimu sana Mwanaume wa Leo maybe kitakusaidia.
Kuna Neema flani mwanamke amepewa na MUNGU ambayo wanaume hawajawanayo,Ana ufahamu mkubwa sana wa kuona mbali kwenye suala la mahusiano kuliko sisi Wanaume,na Ndio maana wanasema katika kila Mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake yupo Mwanamke,Na hii hutokea tu pale utakapo msikiliza."WANAUME HUJENGA MAKAZI LAKINI MWANAMKE KAPEWA UWEZO WA KUJENGA NYUMBA"na ukitaka iwe bora mpatie nafasi yake aitumie ipasavyo kama kweli unampenda.
Ukiona Simu zako kila unapokaribia kufika nyumbani zinakuwa nzito basi ujue unatatizo my friend,Mpe mwache aziangalie kama huna la kuficha na una Mpenda na kumjali hutashinda ukibadilisha "Pattern na Password kila siku"
Kwanini ujitese na wajinga wengine huko nje wakati una Uwezo wa kujitengenezea Amani yako nzuri ndani yako!?
Kumbuka Mwanamke huwezi ukamficha kitu milele as long as Unaishi nae,ni wepesi sana wakuhisi na kufahamu mengi ndani ya nyumba kuliko sisi.
Wengi waliofanikiwa wana urafiki wa karibu sana na wake zao na wanawaheshimu kiuhalisia toka ndani ya Mioyo yao.
Kumbuka huyu unalala nae na kuamka nae kila siku,huoni kama ni ujinga kujishughulisha na viruka njia hivyo vinavyokukosesha amani kwenye inbox za facebook na WhatsApp kila wakati kushinda kuzifuta Message zao kabla hujaingia kwako.Huo ni utumwa wa kujitakia boss."MPAKA PALE UTAKAPO AMUA KUMUHESHIMU HUYO MWANAMKE NDIO BARAKA ZA MAHUSIANO YA NDOA NJEMA ZITA MIMINIKA KWENU"
 
meseji nzuri sana Dada. thanks a lot
 
Ujumbe umeleta mapinduz makubwa sana kwenye fikra zangu nimeamua sasa kufuta mawasiwasi yote kwa mpenzi wangu kesho naongea naye natubu maovu yote naamua kumpa heshima ya dhati na uzur ni kuwa yeye huwa ana niheshimu lakini kuna kosa nimelifanya mwishon mwa mwaka Jana kuna binti flani wa ki mbulu amenichanganha nimemsahau mpenz wangu Mary dah naombeni msamaha sitaki maisha ya kuigiza uaminifu swala la uaminifu ni swala LG kulifanya kweli na sio la kufanya revenge
Nimejifunza kuwa mazungumzo ni njia pekee ya kuchanua penzi lenu pale unapoona matatizo au changamoto au kero the hakikisha unasahihisha mapema na si Kukaa nalo eti ili siku moja uje kuyajumlisha makosa aliyofanya kwa kipindi fulani, come on hiyo haisaidii kitu na hii ni kwasa waliyo tayari kwenye ndoa jaribuni sana kuishi kinyama yaani kila mmoja amtamani kumuuona mwenzake mda wote piga stori na mme wako hata kinafki tu jaman kwani unapungukiwa nini ukijishusha mbele ya mmeo, mnyenyekee mfundishe mpe mapenz kama siku zenu za mwanao
Tamani furaha ile ndani ya ndoa yako
Sote tuna mapungufu lakini pia tuna ufahamu
Asante sista kwa Ujumbe mzuri sana
 
Nimeipenda hii....
 
Hongera kwa kubadili fikra zako juu ya uhusiano wako na kuamua kuona na kuheshimu uthamani alionao mpenzio...

Msamaha ni jambo zuri sana si tu kwa yule anaesamehewa ila zaidi sana na kwako,msamaha ni afya ya moyo wako... Hua najihisi fahari sana na amani ninaposamehe
 
"MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME"
Neno hili Wanaume wengi huwa tunalitafsiri vibaya pale Muhusika anapoanza kuifanya kazi yake Kikamilifu.
Ukiona Mkeo anakuambia "Sipendi na staki uendelee kuchat na wadada flani" au Sina "Amani na Rafiki yako flani naomba uachane nae tabia zake sio nzuri"
Wanaume wengi wa kileo maneno haya huona kwao kama bugudha na hasa huisi wenzi wao wanataka kuwakalia au kuControl maisha yao.
Ngoja nikwambie kitu muhimu sana Mwanaume wa Leo maybe kitakusaidia.
Kuna Neema flani mwanamke amepewa na MUNGU ambayo wanaume hawajawanayo,Ana ufahamu mkubwa sana wa kuona mbali kwenye suala la mahusiano kuliko sisi Wanaume,na Ndio maana wanasema katika kila Mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake yupo Mwanamke,Na hii hutokea tu pale utakapo msikiliza."WANAUME HUJENGA MAKAZI LAKINI MWANAMKE KAPEWA UWEZO WA KUJENGA NYUMBA"na ukitaka iwe bora mpatie nafasi yake aitumie ipasavyo kama kweli unampenda.
Ukiona Simu zako kila unapokaribia kufika nyumbani zinakuwa nzito basi ujue unatatizo my friend,Mpe mwache aziangalie kama huna la kuficha na una Mpenda na kumjali hutashinda ukibadilisha "Pattern na Password kila siku"
Kwanini ujitese na wajinga wengine huko nje wakati una Uwezo wa kujitengenezea Amani yako nzuri ndani yako!?
Kumbuka Mwanamke huwezi ukamficha kitu milele as long as Unaishi nae,ni wepesi sana wakuhisi na kufahamu mengi ndani ya nyumba kuliko sisi.
Wengi waliofanikiwa wana urafiki wa karibu sana na wake zao na wanawaheshimu kiuhalisia toka ndani ya Mioyo yao.
Kumbuka huyu unalala nae na kuamka nae kila siku,huoni kama ni ujinga kujishughulisha na viruka njia hivyo vinavyokukosesha amani kwenye inbox za facebook na WhatsApp kila wakati kushinda kuzifuta Message zao kabla hujaingia kwako.Huo ni utumwa wa kujitakia boss."MPAKA PALE UTAKAPO AMUA KUMUHESHIMU HUYO MWANAMKE NDIO BARAKA ZA MAHUSIANO YA NDOA NJEMA ZITA MIMINIKA KWENU"
Hii ndio nimeielewa
 
We valentina hapo juu kabisa namba moja ingekuwa
*toa hela, toa hela,toa hela, tena toeni hela.
 
Back
Top Bottom