Kubeti kwatajwa kiini cha wanafunzi kufeli

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
HII ya kwamba 'betting' imeathiri matokeo ya Kidato cha IV Dar bado sijaielewa vizuri. Kwamba madogo badala ya kusoma wana-bet au?

C3o6e4bWEAIiCAC.jpg

Nini maoni yako
 
in other hand yes! kumekuwapo na wimbi kubwa la watoto chini ya miaka kumi nane kuingia katika mchezo huu! nadhani ni kipindi muafaka serikali waweke sheria kali kwa hizi nyumba za kubet pindi wanapo admit yeyote aliye chini ya umri
 
Wanashindwa kutulia wafanye tafiti kwa undani wajue nini tatizo!
Kila jitu linakurupuka kutoa sababu za hovyo!

Mara nyingi wanaobet sana ni watoto wa kiume wakike ni mara chache! Sasa je hao wakike wamefanya vizuri?

Utaona matamko yatakavyokuwa mengi!
Sijui nani alituroga!!
 
Mwanafunzi ameingia darasani asubuhi, jana usiku aliandaa mikeka ya mechi za leo ambazo wakati masomo darasani yanaendelea zenyewe zinakuwa zinaendelea pia.

Unadhani hapo mwanafunzi ata-concentrate kumsikiliza mwalimu au kufuatilia mechi zinaendeleaje kwenye mikeka yake?

Dar es Salaam
Dar ndipo kuna makampuni ya kubet mengi mno kuliko mikoa mingine.
Nadhani aliyetoa huo utafiti yupo sahihi kwa kiasi fulani, maana hata shule nyingi za Dar ndio zimeshika mkia.
 
Betting kama madawa ya kulevya, ni ngumu kuacha, we fikiria umeweka jero unaambiwa ukipatia ubashiri wako unakula zaidi za mil. 2, hapo kuna haja ya kuangaika na kusoma badala ya kuombea matokeo yawe kama ulivyotabili.
 
Naweza kuziita hizi ni porojo na "assumptions" zisizo na msingi, kuanguka kwa shule za serikali kumekuwepo sasa kwa zaidi ya miaka 10, hizi ni njia ambazo serikali imekuwa ikizitumia kuonyesha kuepuka lawama na ya kwamba wao sio chanzo cha matokeo mabovu kama vile wenyewe walishafanya kila kitu kinachohitajika katika shule zao za serikali na ndio maana usishangae kuona mwanasiasa akishusha mwalimu mkuu cheo, kama watu hasa wazazi wataendelea kuwa watu kudanganyika na wanasiasa basi matokeo mabovu yataendelea kuwa hivyo siku zote huku mwanasiasa ikiwemo raisi watoto zao wakisoma shule za binafsi zenye ada kubwa na yenye mahitaji yote muhimu.
 
Sidhani
Mi naona ni uzembe wa serikali
Wazazi
Walimu na Wanafunzi
Kwanini zingine zisiwe za mwisho? Je hata hao wadada nao wanabet?
 
Mwanafunzi ameingia darasani asubuhi, jana usiku aliandaa mikeka ya mechi za leo ambazo wakati masomo darasani yanaendelea zenyewe zinakuwa zinaendelea pia.

Unadhani hapo mwanafunzi ata-concentrate kumsikiliza mwalimu au kufuatilia mechi zinaendeleaje kwenye mikeka yake?

Dar es Salaam
Dar ndipo kuna makampuni ya kubet mengi mno kuliko mikoa mingine.
Nadhani aliyetoa huo utafiti yupo sahihi kwa kiasi fulani, maana hata shule nyingi za Dar ndio zimeshika mkia.
Umeambiwa wanao beti ni wavulana je wasichana wamefaulu?
 
kwa hiyo watoto wa kike wamefauli sana dar kushinda wanaume wanao-bet?
 
Eti anatafutwa mchawi!!!! Halafu akapatikana ni kubeti.
Siyo ukosefu wa walimu, walimu wenyewe kupuuzwa, mahitaji kutoenda kwa wakati muafaka, ubovu wa sera na usimamizi wake? Hapana ni kubeti.

Manina
 
Umeambiwa wanao beti ni wavulana je wasichana wamefaulu?
kwa hiyo watoto wa kike wamefauli sana dar kushinda wanaume wanao-bet?
Mara nyingi darasa likiwa na wavulana wasiojielewa, lazima huo ujinga wa wavulana uwaathri hadi wasichana, ni wasichana wachache mno watakaopona. Ila darasa likiwa na wavulana serious, wasichana huwa wana-behave hata kwa ku-pretend tu!
 
inawezekana imechangia kwa namna moja ama nyingine,lakini ukweli ni kwamba kuna sababu nyingi na kubwa zaidi kuliko hiyo ya kubet..mojawapo ya sababu hiyo ni serikali yenyewe haijaweka utaratibu au mfumo mzuri wa ushiriki na support ipasavyo katika elimu.
 
Wanafunzi wa siku hizi mapenzi mengi, siku zote mshika mawili moja humponyoka. Maana nikikumbuka mwaka wetu sisi wakati tupo skuli na Wadau wang tulikuwa tunasema " mixuli kwanza mapenzi no "
 
Nakumbuka nilikuwa natia mixuli mpaka nasahau kuoga alafu asubuhi nikiingia skuli najikuta nna mswaki kwenye mfuko wa suruali ya shule daah ulikuwa nomaaaa
 
Back
Top Bottom