Kubet ni dhambi?

Katika Ulimwengu hakuna dhambi hizo ni porojo za Wazungu na Waarabu tu. na Imani zao za sungura na fisi . Tunachokaza Waafrika ni kwamba Watu hawatakiwi kuishi kwa kubahatisha tufanye kazi.Wazee wa Kiafrika wanasema Michezo ya kubahatisha ni burudani tu wale usiwekeze akili huko maana mwanya wa kufanikiwa ni mdogo sana
 
Mkuu unasema kwenye riba hakuna hasara upo serious kweli ??

Waulize wanaofanya biashara ya kukopesha kama hawapatagi hasara
Kunakuwa na collateral security (Bond/Rehani) ku- secure huo mkopo, mdaiwa akishindwa asset inauzwa ku-cover loss.
 
Kumbukumbu la Torati 18:10
[10]Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
 
Kumbukumbu la Torati 18:10
[10]Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
Ushawahi kusoma Hilo andiko katika Biblia ya kiingereza ????? Ukaona neno lililotumika kubashiri ni neno gan?

Deuteronomy 18:10
There shall not be found among you any one that maketh his son or his daughter to pass through the fire, or that useth divination, or an observer of times, or an enchanter, or a witch,

Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

Sasa unajua maana an enchanter?

enchanter from oxford dictionary
noun
a person who uses magic or sorcery, especially to put someone or something under a spell.

Yapo maneno mengi kwenye kiswahili huwezi pata tafsiri halisi iliyokusudiwa jizoeze kusoma maandiko Kwa lugha tofaut hasa zile ambazo ndio zilitumika kuandika Kwa matoleo ya kwanza.

Maneno mengi sana kwenye Bible ya kiswahili yanaleta shida sana watu wakiyasoma.

Kwa kumaliza tu hiyo bashiri iliyotumika hapo sio betting ni bashiri za wapiga ramli

Ramli ni neno la kiarabu ambalo Huwa matumizi yake ni watu hutumia kumwangalia mtu ana matatizo au shida Gani. Ndio kilikatazwa hiko .
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…