Kubet ni dhambi?

kubeti ni kama uzinzi, wizi au ulevi

ni kama familia au jamii ya watu wazinifu, mashoga, wasagaji na makundi ambayo yanapambana kwamba wanachokifanya ni haki yao halali na sio dhambi.

watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...
Kwa kukosa maarifa 🤣🤣🤣 marifa yakowapi?tupe eleza dhambi inatoka wapi ?Wewe hapo usipobeti huwezi ukakizi mahitaji yako ya kila siku.
 
Onyesha proof
proof ya nini tena?

Mashoga wanatafuta uhalali kwamba wanachofanya ni haki yao na ni halali haina shida kabisa....

Wabetiji nao ni hivyo hivyo...

Ndio maana kuna wanaoona ni sawa na kuna wanao ona si sawa...

Akili za kuambiwa changanya na zako...
 
proof ya nini tena?

Mashoga wanatafuta uhalali kwamba wanachofanya ni haki yao na ni halali haina shida kabisa....

Wabetiji nao ni hivyo hivyo...

Ndio maana kuna wanaoona ni sawa na kuna wanao ona si sawa...

Akili za kuambiwa changanya na zako...
We mtu Akiwa shoga nini kinabadilika katika maisha yako, same as betting, hawavunji sheria, hii sio Afghanistan sio kila mtu anamuamini Mungu wako wa kiarabu... heshimu mipaka ya watu
 
Kubet ni kamari,kamari ni Haram, QUR'AN 5:90
 
Naona unavyohangaika kuhalalisha KAMARI mkuu.

KAMARI NI DHAMBI KWA DINI HIZO MBILI (ACHA KAMARI).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Sio dhambi , leta kifungu kinachosema ni dhambi ,reference iwe bible au au Quran
 
Sasa wewe unazungumziaje swala Zima la kubet especially sports betting maana ndio ambayo imekuwa habari ya mjini Leo hii ni Halali au si Halali Kwa misingi ya dini?
Kamari ni dhambi, alafu Mungu hataki watu wanaomuabudu waishi maisha ya kubahatisha maana na yeye hafanyi mambo kwa kubahatisha.
 
Kuna afisa ubashiri aliwahi kuleta kifungu cha biblia kinasema tafuteni pesa hata kwa kubashiri.
Kifungu chenyewe nimesahau.
 
Yale yale ya Profit(faida) na Interest (riba). Watakuambia riba ni haramu lakini faida ni halali. Lakini ukifuatilia vizuri utagundua kuna tofauti ndogo sana kati ya riba na faida
Kuna kitu kinaitwa factors of production (Nyenzo za uzalishaji mali). Theory of distribution/Price Indices.

Kila nyezo ya uzalishaji mali ina ujira(reward)wake.

-Labour-(Salary/Wage)
-Land-(Rent)
-Capital-(Interest)
-Entrepreneur-(Profit/Loss)

Sasa kwa mtiririko huo tofauti ya riba na faida tutaibaini kwamba, huyo mjasiliamali(enterpreneur) sio mara zote anapata profit/faida, kuna muda ana incur loss/hasara, lakini kwa anaeweka Capital/mtaji ili apate interest (riba)yeye lazima apate faida yeye hanaga hasara, ila wa profit anaweza pata mara dufu ya kile alichoweka na wa interest yeye iko fixed kwa muda maalumu, kama ni 5000 kwa mwezi au kwa mwaka kiasi ni kilekile hakipungui wala kuzidi(fixed percentage over time).
 
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema:-

"Katika hivyo mna madhara makubwa na (baadhi ya) manufaakwa (baadhi ya) watu.Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake." (Al-Baqarah 2:219)

Hakika Sheitani anataka kukitilieni uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari.........."(Al-Maidah, 5:91)

Ni dhahiri kuwa mcheza kamari anayeshindwa na kupoteza fedha zake, huhamaki na kughadhabika kwa kumwona mwenzake akitumbukiza fedha hizo zote mfukoni mwake huku akicheka kwa furaha ya ushindi wake. Hivyo hasira na ghadhabu hizo huja wakati mmoja zikatokeza na kusababisha maafa makubwa.
 
Let
hata nikishusha aya za bibli zinazokataza kamari hutaelewa utabaki kupinga tu
Kama wewe, unavifungu viweke hapa sio lazima mimi ni elewe lakini sababu jamii forum ni platform ambayo ni accessible kwa wengi utafanya wengine waelewe Yale ambayo maandiko yanasema.
 
Kila kitu kwenye maisha ni kubeti,na kubeti sio dhambi.kubeti Ni Kama ofisi zingine unafanya Kazi na unapata mshahara wako,,
Naunga hoja mkuu,
Mkuu ONJO,
kitu chochote kile ambacho unafanya hujui ni kwa namna gani unapata pesa kina implication kubwa sana kwenye maisha yetu haswa sisi Vijana.

Betting ina negative implications kubwa sana, kwanza inaaminisha ubongo kuna njia rahisi ya kupata pesa pasipo kuelewa mchakato mzima wakupata pesa hiyo.

Huwezi fananisha betting na biashara ya kuuza mchele mfano, mfanyabiashara anaenda kujumua mzigo kiroba cha kg100 kwa kiasi fulani then anakuja kuuza kilo1 kwa kiasi fulani at the end unafahamu mchakato mzima wa kuingiza pesa.

Halafu huwezi kusema betting ni sawa na Mshahara, hilo haliwezekani! Una mkataba wa miaka5 kampuni X kila tarehe 23_29 mshahara wako kiasi cha shilingi Milioni1 kinaingia, unaweza kusema kila tarehe hizo nitabet nitaingiza kiasi cha shilingi kadhaa?

Sijaegemea angle ya dhambi, ila kuna vitu vinaharibu sana. Hasa hizi pesa tunazoaminishwa ni za kubahatisha.
 
Kwa kweli hii michezo ya kubeti ni ya kupigwa vita mpaka ipotee, ni uchezeaji wa hela na tamaa ya kupata hela kwa njia ya shot cut. Ni upotevu wa fedha, anayepata ni mwenye kampuni ya kubeti. Wizi mtupu wa kijanja
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…