Kubenea: Tumeokoa 1.2 bilioni za ufuaji majoho ya madiwani

abackuk

Senior Member
Jan 6, 2014
194
190
  • Kubenea ameyasema hayo leo wakati alipofanya mkutano wa hadhara uwanja wa Mabibo Farasi ikiwa ni ziara ya kwanza jimboni kwake tangu achaguliwe Oktoba 2015.
  • "Ubungo tumeokoa Sh 430 milioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho 18 ya madiwani, Kinondoni Sh 800 milioni kwa majoho 58 na tangu Aprili mwaka jana hatujafua na hatujatoka upele," amesema Kubenea.
  • MY TAKE:chukulia ubungo pekee majoho 18 kwa 430milioni kwa mwaka.Ina maana kila joho moja kwa mwaka ni takriban 23.8mil,mwaka una wiki 52 kwa hiyo kila wiki joho moja lilitafuna milioni takriban 495,000/=(assuming kwamba kila wiki joho linafuliwa).
  • YALIKUWA MATUMIZI SAHIHI YA PESA ZA UMMA?

Chanzo gazeti la mwananchi
 
Hii nchi ina safari ndefu. Watu wengi hupata fedha zao kwa njia zisizohalali. Ni mkato mkato kwa kwenda mbele.
They dont produce the value for what they earn...
 
Aisee ccm wametunyonya sana na bado tunanyonywa kwel kwel.... Bora arudi mjerumani na bakora tuu....( hensrani) tungenyooka tuu
 
kubenea kwa fix? joho jipya sh ngapi maana hata wangebadili kila week wavae jipya sidhani kama ingefika hela hiyo
 
kubenea kwa fix? joho jipya sh ngapi maana hata wangebadili kila week wavae jipya sidhani kama ingefika hela hiyo

Siyo uongo ni kweli kabisa.MWansheria wa HALMASHURI moja alikuwa nalipwa kila kikao Tzs500,000 ya suti mpya
 
Maajabu haya,..
Yaani joho lile hata omo ya 200 haiishi, lilikuwa likifuliwa kwa lak5 kwa wiki?
 
Yalikuwa yanapandishwa KLM au Emirates kwenda kufuriwa, tena hapo huyapeleki kama mizigo, unayakatia siti business class kila moja linafunga mkanda kwenda kufuliwa kwa bibi malikia.
 
Kuna watu walikuwa wanapata hela kama wachukua tenda za serikali? Rim kkoo inauzwa6000 ila wao wanauza mpaka elfu kumi muda huo lakini, rafiki yangu aliomba tenda moja hivi akaambiwa atoe milion hamsin ili apate
 
Hivi kikao kilichopitisha bajeti hii, Mnyika na Mdee kama madiwani kwa vyeo vyao vya ubunge, walishiriki?
=====
Mbona Gazeti la Uhuru halikufichua matumizi mabaya haya? Hivi gazeti hili makini na waandishi wao waliobobea walishindwa Kuipata hii kweli kipindi chote hicho?
 
  • Kubenea ameyasema hayo leo wakati alipofanya mkutano wa hadhara uwanja wa Mabibo Farasi ikiwa ni ziara ya kwanza jimboni kwake tangu achaguliwe Oktoba 2015.
  • "Ubungo tumeokoa Sh 430 milioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho 18 ya madiwani, Kinondoni Sh 800 milioni kwa majoho 58 na tangu Aprili mwaka jana hatujafua na hatujatoka upele," amesema Kubenea.
  • MY TAKE:chukulia ubungo pekee majoho 18 kwa 430milioni kwa mwaka.Ina maana kila joho moja kwa mwaka ni takriban 23.8mil,mwaka una wiki 52 kwa hiyo kila wiki joho moja lilitafuna milioni takriban 495,000/=(assuming kwamba kila wiki joho linafuliwa).
  • YALIKUWA MATUMIZI SAHIHI YA PESA ZA UMMA?

Yaani joho moja ni sawa na Tzs 23,888,888 wakati watoto wanakaa chini shuleni, hospitali hazina dawa, shule hazina vyoo, wanafunzi wa elimu ya juu hawana mikopo?
 
Unaposema umeokoa 1.2billion utupe na mchanganuo wa matumizi ya hiyo pesa kama alivyofanya JPM alivyookoa pesa za sherehe za wabunge na akaamua kuzipeleka muhimbili kununulia vitanda vya wagonjwa. Sasa hiyo 1.2billion baada ya kuokolewa imeenda wapi?
 
Back
Top Bottom