Kubenea: Kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Zanzibar, waandishi hawaruhusiwi kuandika

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968


Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amedai kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kisiwani Pemba na waandishi wa habari wa kujitegemea wanazuiwa kuandika kwa kunyang'anywa leseni, ametolea mfano mtangazaji wa DW kunyang'anywa leseni ili asiripoti matukio yanayotokea.

Amesema waandishi wa habari waende Zanzibar na kujionea kisha waripoti na sio kukaa na kusikiliza serikali inaposema wapinzani ni wakorofi halafu ndio kuandika
 
Tuma waandishi wa MWANAHALISI wakaandike nani anayetaka kumwagiwa tindikali ya usoni sasa hivi.
 
Akihojiwa na DW amerudia maneno ya Jenerali Ulimwengu kwamba taifa limerudi nyuma miaka 50 kwe demokrasia. Amesema kule Pemba hali inatisha na waandishi wameogopa kwenda kuripoti yanayoendelea huko.

Amesema wabunge wa upinzani wameamua kuwalipia nauli na gharama nyingine ili waende kama kundi ili wakusanye ushaidi utakaosaidia kuipeleka serikali mahakama ya kimataifa ya uharifu dhidi ya binadamu. Amekemea pia kitendo cha polisi kumnyanganya kitambulisho mwandishi wa DW.

Amesema waandishi watanzania wamejaa hofu maana siku hizi wanapigiwa siku za vitisho wakielekezwa cha kuandika. Amesema sasa wameamua waanze kupiga kelele ili dunia ijue kinachoendelea nchini.
 
Nchi imepiga about turn ya ghafla katika demokrasia na sio ajabu ikaingia kwenye orodha ya nchi hatari.
Kama serikali ifanyayo ni mambo mazuri hofu ya juweka wazi inatoka wapi?
 
Kubenea bwana sasa si kapeperushi kake ka mwanahalisi kapo? Mbona hakaandiki?

Alizoea kuandika uongo sana huyu jamaa....
 
Tatizo uandishi wao upo kama ule uliokuwa wa kumshambulia waziri mkuu mstaafu kwa kashifa ya r kumbe hakuwa na kashfa ilikuwa uzushi wa mwandishi na mhariri mkuu!
 
Shida ya serikali hii haitaki kukosolewa wakati, ukikosolewa mdo unaimarika kisiasa, hii ni hatari
 
Nimependa sana elimu yake ya hapa na pale iingizwe kwny utaratibu
Hivi uliwahi kujishughulisha kujua elimu ya Mh Kubenea , au umekaririshwa tu ? Hushangai walikopotelea wachumia tumbo wenzio waliokuwa wanahoji elimu yake !
 
Kubenea anatafuta kick,mbona yeye anavumiliwa na uandishi wake wa habari wa hisia na habari zisizobalance
 
Huyo mwandishi wa kimataifa kwa nini kanyimwa kibali? Au ni mchochezi kama Kubinyua? Wa kimataifa anafanya nini Pemba huku wenziye wako BREXIT na California? Pemba?
 
Ina maana wananchi wa Pemba hawana hata smartphones ama hawashiriki katika social medias kama instagram and the likes?! Dunia ya sasa kweli is it possible kuwa contain binaadam kiasi hicho?
 


Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amedai kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kisiwani Pemba na waandishi wa habari wa kujitegemea wanazuiwa kuandika kwa kunyang'anywa leseni, ametolea mfano mtangazaji wa DW kunyang'anywa leseni ili asiripoti matukio yanayotokea.

Amesema waandishi wa habari waende Zanzibar na kujionea kisha waripoti na sio kukaa na kusikiliza serikali inaposema wapinzani ni wakorofi halafu ndio kuandika

Huyu mbunge ni mjinga wa kiwango cha phd. Ukisema vyombo vya habari binafsi hata na wandishi wao ni binafsi kwa maana hawana fungamano na serikali. ITV inaye Faroq Karim, Channel Ten wanaye Munir Zacharia na Star Tv wanaye Pandu wote wanafanya kazi zao na kila siku wanatoa taarifa mbalimbali zinazotokea Zanzibar.
Huyu mwandishi anayemsema ni nani? Hiki chombo cha DW wakati wa uchaguzi wa marudio mwandishi aliyekuwa akiandikia chombo hicho na gazeti la Mwananchi alidai kutekwa. Kwa huu msuguano kwa mwandishi kupata adhabu ni sahihi.
 
Fani zingine za kitaalamu mtu hapewi leseni ya ku-practice taaluma bila kuwa na digrii.Uandishi wa habari limekuwa jalala la kila mtu hata kubenea na elimu yake ya kuunga unga ruksa kujiita mwandishi wa habari ruksa.

Hiyo fani wakitaka ikae vizuri leseni ya uandishi wa habari na utangazaji itolewe kwa watu wenye digrii tu.Wasigawe leseni tu hovyo kama wanagawa kondomu
 
Back
Top Bottom