KATIBU TFF
Alipotafutwa na gazeti hili jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema malipo ya asilimia 15 ya uwanja katika mgawo wa serikali kutokana na mapato ya mechi zinazochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wanayafanya kwa fedha taslim kwa kuwa
wizara yenye dhamana ya michezo nchini iliomba yafanywe kwa njia hiyo
kwa madai kuwa fedha hizo zina matumizi ya haraka.
"Sisi (TFF) tulipanga kuwa tunawalipa kwa 'cheque' (hundi) lakini wizara ilituomba tulipe kwa fedha taslim kwa sababu
mfumo wa hundi huchukua muda fedha kumfikia mlengwa na wao (wizara yenye dhamana ya michezo)
walidai fedha zao zina matumizi ya haraka," alisema Osiah.
"Nafikiri mfumo huu wa malipo ya fedha taslim utabadilika tutakapoanza kutumia teknolojia mpya ya tiketi za elektroniki msimu ujao maana malipo yote yatakuwa yanafanyika benki," aliongeza Osiah.
Source :
Home