KUBANA MATUMIZI KUMEWABANA PUMZI

Abtali mwerevu

JF-Expert Member
May 5, 2013
652
492
KUBANA MATUMIZI, KUMEWABANA PUMZI
Wote wanaolia na sera ya kubana matumizi, ni vigogo, wenye vitambi laini vilivyojaa mafuta ya dhuluma!!

Wamiliki wa mahoteli makubwa, wanalia biashara imekuwa ngumu, vikao vya mawaziri vimezuiwa hawapati wateja tena. Je kuna ubaya wowote wamiliki hawa wakikosa, mkulima alimaye kwa jembe la mkono naye akapata visenti kadhaa?


Wauza pombe wanalalamika, bana matumizi ya serikali imesababisha wateja wapunguze idadi ya bia! Je ni taifa lipi lilijengwa na walevi?

Akifanyiwa mahojiano na gazeti la Mwananchi, Ndugu Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje alisema haya,
"lazima waziri wa mambo ya nje awe nje ya nchi kwa muda mwingi na ikitokea yuko ndani ya nchi kwa mwezi mmoja mfululizo, lazima ni mgonjwa."
Huyu siwezi kubishana naye kwa maana kastaafu siasa, lakini sidhani kama ni busara kutetea ANASA!!
 
Heshima inarudi taratibu!! Siku hizi hakuna kufunga bar. Kuna kipindi kibosile fulani alinunua vilevi vyote kaunta,mabibi 3 pembeni,tukanyimwa huduma sisi wa bia 2.
 
Back
Top Bottom