Kubadilisha mwanamme inawezekana!?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Kumbadilisha mwanamme inawezekana!? (
Natumai umzima. Leo nakukaribisha tena shosti, tumalizie makala hii nikiwa naamini kuwa umekuwa na hamu kubwa kutaka kujua mwishilio wake ukoje.


Wiki iliyopita msomaji mpya, tuliuanzisha huu mjadala hapa, wa "Kumbadilisha mwanamme tabia"

Wengi watakwambia "kumeza kiwembe nirahisi kuliko kumbadilisha mwanamme".


Mathalani iwe ni mvutaji sigara, mlevi chakari au labda iwe ni mgonjwa wa wanawake yaani kwa lugha nyingine kicheche, Namna ya kumbadilisha niamini ni ngumu.


Ukweli ni kwamba Mwanamme huwa habadilishiki tena si kwa usiku mmoja usijidanganye shosti wangu, mwanamme anaamua mwenyewe kubalika na si kwakubadilishwa, tena sio na wewe.


Kama nilivyosema wiki iliyopita kuwa ni vigumu kumbadilisha mwanamme kwa kuwa unapojaribu kufanya hivyo Daima atakupinga. Kubadilika kwake kunakuja atakapo kaa amini kuwa madhara yatokanayo ni mabaya kwake na si kwasababu ya kumridhisha mtu fulani.


Mayunga mwanamme wa makamo anasema; "Mke wangu alikuwa hapendi nivute sigara lakini nikwa navuta nje nikija nyumbani nakula pipi ya kifua, ikaenda mpaka sikumoja nikashikwa na kifua kikali nilipofika hospitali nikaambiwa ni kwasababu ya sigara, nikaacha hapo hapo."


Anasema indapo mkewe angechukua njia sahihi za kumkataza angeacha lakini kwa kua alikuwa anatumia ukali kwa hiyo moyoni alihisi kama kutii moja kwa moja ni kama kujishusha kwa mkewe.


Huyo ni Mayunga. Lakini karibu wanaumme wengi watakwambia kuwa wanawake hawajui namna ya kumfanya mume aache kitu ambacho kimemganda. "Wanafanya kama wanashindana nasi," anasema Michael. Usichojua ni kwamba unapojifanya unakua mkali kwa kitu fulani kama hicho basi mwenzako anajifunza kuwa muongo smart.


Ni sawa na unapojaribu kumpindisha kwa nguvu mwanamme hapo ndipo unapokosea kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kutaka kuyanyoosha matege ya mtu mzima.

Chakufanya mpe nafasi ya yeye mwenyewe kubadilika utaona matokeo.


Unaweza pia kumshirikisha mtu ambaye unajua yeye anamheshim na anaweza kukusaidia kumbadilisha tabia ya mumeo.


Wakati mwingine pia kwa kukita goti chini kumuomba Mungu Mume atabadilika. Mwisho kabisa Kuwa kama mshauri wake au kama rafiki yake lakini si kama mama yake.


Naamini pia kuwa mwanamme anabadilika kutokana na muda na mapenzi ya kweli. Lakini pia ni vizuri kuzungumza naye..! na hii kila siku huwa naisema, Mazungumzo bwana ni power. Hata kama kuna tatizo utatuzi utakuja endapo mtazungumza. Halalala ungea naye taratibu shosti utaona jinsi unavyoweza kumbadilisha.


Ni hayo kwa leo na kama kuna maswali usisite kuniuliza kupitia
 
sijua ana taka badiliko gani?
1. La umbo? (physical change)
2. La kikemikali ( Chemical change)

F.2 kama sikosei, mtoa.mada tafut nDAFTARI LAKO LA F.2 chemistry....!
 
Sio mwanaume tu hata kumbadilisha mwanamke ni shida pia. Hatuoani au kua kwenye mahusiano kwa lengo la kubadilishana tuanzie hapo.
Kubadilika ni vile mtu anaona mwnyw. Mimi vitu uanaweza ni badilisha kirahisi ni kuwa negativu maana shetani anaweza kukusaidia mfano mimi sipendi kuchelewa ila ukinikorofisha naamia kwa washkaji zangu tutaonana weekends tu!
Pombe na sigara sio ishu kwangu siwezi kabisa. Mademu ukinipa gap inawezekana tena kwa mbali sana.
 
Back
Top Bottom