dogo umenikumbusha kipindi nimemaliza,mie pia nilipata 2 na kombi zote zilikubali,ila nikachaguliwa kwenda DIT mimi nikawa nakataa kabisa nikafanya na mipango ya kubadilisha bila kusema nyumbani kwani nyumbani wazazi walifurahi sana mimi kupata collage mwishoni kikaitwa kikao cha ndugu na jamaa wote ili wanishauri baada ya kujua kua mie sitaki kwenda DIT wakanipiga mkwara sana na kuniambia kua nikienda 6 hawatanilipia ada wala hela hawatanitumia
ikabidi niende DIT.kitu nilichofanya pale ilikua ni kupiga misuri,kipindi namaliza nikapata ajira moja kwa moja,nikawa napata hela ya kutosha kimaisha ya ujana ilikua kama laki 7 kwa mwezi,wazazi wakaanza kuniambia tulikwambia sasa bila cc kukukata usiende 6 ungekua unapata wapi hizo hela,wakati huo marafiki zangu walioenda 6 ndo walikua waingia chuo mimi niko kazini wakawa wananitamani sana mpaka wakawa wanajuta.
matokeo yalitoka mazuri nikaomba vyuo kama 3 bongo na 2 nje vyote nikapata nikaona niende nje,uko walipoona kuna vitu vingi ninavijua wakanirusha mwaka nikamaliza sawa na wale watu wa 6 walioingia chuo ngoma ikawa droo
niliporudi kuanza kutafuta kazi mimi nikawa napewa kipaumbele kuliko wale wa 6 kwani nilikua na experience ya kazi,nikaanza kuchagua wapi watanilipa vizuri.
sasa kwa ushauri wangu wewe nenda DIT kama utachaguliwa uko ila kafanye shule pale sio kwenda kufukuzia watoto wa shule na madem wa CBE.