Kubadili mawazo ni kitu cha msingi sana

Aug 29, 2020
1
2
Mawazo ni kitu cha msingi sana katika maisha yetu.Mawazo yana nguvu kubwa.

Mawazo yakiunganishwa na malengo yanayoeleweka,subira pamoja na Nia yatatusaidia kufikia mafanikio na utajiri.

Watu huwa tunapitia hali ngumu mbalimbali katika maisha,kwa mfano.
1. Umaskini.
2. Kukosa nafasi za ajira.
3. Kukosa pesa.
4. Kufeli katika maisha.
5. Kukosa ushauri mzuri wa mafanikio.

Hayo yote yanawafanya watu wakose kuwa na utulivu wa mawazo mazuri kuhusiana na kuwa na malengo yanayoeleweka.

William James alisema "Mtu hatabadili maisha yake kama hakuanza kubadili fikra zake".

Mojawapo ya changamoto kubwa inayowakabili watu ni kukosa kuamua kwamba nini tunahitaji katika maisha.
Tafakari huwa unafikiria nini unahitaji katika maisha.

Na
Hosea Justine Simwogope.
Think well,Speak well and Do well.
 
5😔 shida inakuja wabongo wengi tumeridhika na umaskini. So kukutana na watu wenye vision moja ni ishu
 
Back
Top Bottom