Kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu Zanzibar na Changamoto za Utawala Bora

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Wana JF hili mnalionaje?

Mh. Rais wa Zanzibar Dr. Shein amemteua na kumwapisha Mh. Omar Othman Makungu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Mh. Makungu alikuwa ni mmoja kati wa makamishina/wakurukenzi wa Tume ya uchaguzi wa Tanzania (NEC).

Binafsi naona ukiukwaji mkubwa wa misingi ya utawala bora. Huyu mtu alikuwa ni kiongozi wa juu kabisa wa tume ya uchaguzi, ambayo katika mazingira ya kawaida tuliitegemea kuwa huru na kuendesha shughuli zake bila kuegemea wala kupendelea chama chochote cha siasa.

Je tutajiridhisha vipi sisi wananchi kwamba Dr. Shein hajamteua Bw. Makungu kuwa mwanasheria mkuu kama asante/shukrani baada ya 'kazi nzuri' waliyoifanyia CCM na JK hasa ukizingatia wingu lililotanda nchi nzima juu ya tume kuchakachua matokeo ya uchaguzi?

Kwa namna yoyote ile, huwezi kumtofautisha Dr. Shein na CCM au Dr. Shein na JK. Je labda ni ahadi waliyopewa viongozi wa tume kwamba wakifanikisha 'dili' basi CCM watahakikisha wanawapa viongozi wa tume kifuta jasho?

Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na katiba mpya itakayoweka miongozo mizuri juu ya taasisi muhimu kama hizi. Ningetarajia kuwa katiba ingewazuia viongozi wote wa juu wa tume ya uchaguzi kutoruhusiwa kuteuliwa na Rais katika nafasi zozote zile za utendaji kwani kinyume na hapo ushawishi wa rushwa ni mkubwa sana.


Binafsi napata shaka sana na uteuzi huu.
 
Kusema kweli uteuzi wa Makungu unatia shaka, lakini ndio limeshafanyika. La kufanya ni kuona atakuwa mwadilifu kiasi gani. Lakini kwa upande mwengine uteuzi wake unanipa moyo pale alipozua hoja ya "kuwabebesha mzigo mkubwa wapigakura Wazanzibari" kwa kuwafanya wachague watu watano siku moja, yaani Rais wa ZNZ, Mwakilishi, Diwani, Rais wa TZ na Mbunge. Hapa ndipo nitaoona uadilifu wake, yeye akiwa Mwanasheria wa Zanzibar anauwezo wa kuibadilisha hali hii, lakini ikiwa alisema yale kwa kujipendekeza tu, vilevile tutamwona. Mwisho wa yote, Mungu hamfichi mnafiki.
 
Tazama hii video kuanzia dakika ya 27

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom