Kuanzia leo naacha pombe

Hesabu zako kali sana

hizo pesa ulizochangia pato la nchi (usizilalamikie sana)

chamuhimu saivi angalia usije ruka mkojo ukakanyaga Uharo.

Maana wengi wanaojaribu kuacha wenyewe Hutoka ulevi A na kuhamia ulevi B(KUWA MAKINI HAPO).

ile pesa uliyokua unaitumia kila wiki 138,000 hakikisha kila wiki unapeleka BANK(kwenye fixed account) hiyo pesa.

Yani hakikisha tena bila kuangalia pembeni BANK kila wiki inaingia ile 138,000...

mwakani tarehe kama ya leo tar 05/11 Toa hela yote uliyojiwekea kwa uaminifu mkubwa sana.

Utakua ni kama jamaa lililo shinda JACKPOT then hiyo PESA yote sasa ya mwaka mzima kama ulivyosema 134,550,000.

Fanyia kitu kama MEMORY ya pesa uliyokua unapoteza kwenye pombe so JENGEA (nashauri JENGEA) then hiyo nyumba

uje uwasimulie wanao/wajukuu ilikuaje na imetokea wapi utakua umewaokoa wao mpk na vizazi vyao na utawapa Fundisho

kubwa sana katika maisha yao.

ILA KAMA BAADA YA KUACHA POMBE

hutoweza tena kusanya hiyo hela kupeleka BANK aseee nakushauri RUDI TU kwenye pombe maana Pombe ina faida

kwako kuliko hasara....yani kama utashindwa tengeneza hiyo amount kwa wiki,kwa mwezi,kwa mwaka Haina haja ya wewe

kuacha pombee ndelea tu kuzinywa maana inaonyesha POMBE hukupa mzuka wa kuchakarika kuliko utapoiacha.
 
Acha uongo huwezi ukanywa kila siku, we wiki nzima pombe tu, angalia sana familia yako isije kukushinda
 
Aisee noma sana,na hapo bado hujamnunulia mwajuma Supu na pesa ya kuhonga pia hujatoa.

Kwakweli pombe na wanawake ni hatari sana

BTW Hizo pesa usipozitumia kwenye kitu ambacho unakipenda ulikuwa unataka uzipeleke wapi kwa mfano.?
 
UMENENA KWA FIKRA YAKINIFU!

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Hahahha nacheka utadhani mazuri.. ila all in all nimepitia situation kama yako.
Amini usifikirie pesa tu. Fikiria mambo mangapi umeyaepuka wakati unakunywa hiyo pombe. Its rather utumie elfu 20 leo kuliko kujiweka katika janga la maisha yako yote. Hope u know wat i mean
 
Nakuomba kwa mustakbali wa taifa letu changa usiache kunywa hiyo kitu. Serikali ina shida sana na kodi ulipazo kwa kupitia kinywaji ukipendacho . Watoto wetu bado wanahitaji matibabu na madarasa ya kusomea. Tunahitaji barabara za lami kilometa zote nchini. Nakuomba usiache kunywa.
 
Labda ungepiga hesabu na deal ngapi au watu wangapi wa maana uliokutana nao huko unapokunywaga.

Wakati mwingine faida ya pombe sio kinywa tu je imekuunganisha na watu wangapi au deal ngapi?
 
Sasa ukitaka kujua Dunia ina mambo na maajabu, ukiacha pombe tuu na hizo hela unazodhani ulikuwa unapoteza zinapotea na hupati tena, pia hata michongo inaanza kufa😀😀😀
 
Hongera lkn nadhani maisha tukifanya calculation ya namna hiyo tutakufa kwa pressure

Muhimu punguza marafiki wanaokudefine hapo utasogea
 
Drink until you are in critical condition eg hepatitis, cirrhosis and other kind of heart disease.
It when you'll quit it easily.
Good luck
 
We acha kunywa pombe uone kama utaona umhimu wa kutfta izo helaaaa.yaaan nyie ndio mnakujaga hapa kusema umelogwa
 
Hatua ya kwanza ni kujua tatizo hatua ya pili ndio huwa ngumu yani kupambana na tatizo au kulisuluhisha tatizo Mimi binafsi nimetumia herb kuachana na ulevi so now na meditate tuu no hangover
 
Amelaaniwa yule anywaye pombe mithili ya kunywa chai
 
Bora umeshitukia..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…